Wednesday, 28 March 2018

JESHI LA POLISI MKOA WA GEITA LIPO IMARA KUDHIBITI UHALIFU NA MAANDAMANO APRILI 26



Jeshi  la polisi mkoani Geita , limewataka  wananchi  katika kuelekea   siku kuu ya pasaka pamoja na uzinduzi wa mwenge Kitaifa, kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na wazazi kuhakikisha usalama na watoto  wanapokuwa kwenye maeneo ya barabara na mitaani.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya jeshi la polisi Mkoani hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Mponjoli Mwabulambo alisema katika kipindi hiki cha siku kuu ya pasaka wameimarisha ulinzi na kwamba hakuna mwananchi atakayesumbuliwa kwenye kipindi chote cha siku kuu.

“Niseme tu kwamba tumejipanga vya kutosha kuhakikisha kila sehemu inakuwa salama na pia niwaombe watu kusherekea kwa amani siku kuu ya pasaka na kwa Yule ambaye hataonekana kutaka kuvunja amani sheria kali zitachukuliwa dhidi yake”Alisema Kamanda Mponjoli.

Kamanda Mponjoli pia amewata wazazi na walenzi kuwa makini na watoto wao na kuhakikisha wanawachunga kwenye kipindi cha siku kuu huku akipiga vita suala la disko toto.

Sanjali na hayo Kamanda Mponjoli, amewatahadharisha watu ambao wamepanga kuandamana  tarehe 26 april kuachana mara moja na suala hilo na kwamba wamejipanga vyema kulinda amani ya Mkoa na mtu yeyote ambaye atabainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

No comments:

Post a Comment