Baraza la madiwani wa halmashauri ya
mji wa Geita,Wilayani Halmashauri ya Mji Geita limepitisha makadirio ya
bajeti ya matumizi ya ya mwaka wa fedha 2018/2019 kiasi cha shilingi Bilioni
44,983,764,197.00 katika shughuli mbalimbali za Halmashauri. Kati ya Fedha hizo
Jumla ya Tsh 15,585,248,344.00 ni kwa ajili ya shughuli za Maendeleo
ikiwa ni Mapato ya Ndani, Ruzuku ya Serikali na Wahisani mbalimbali.
Tshs. 4,765,976,688.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikiwa ni Ruzuku kutoka
Serikali kuu na Mapato ya ndani na Tshs. 24,632, 539,165.00 kwa ajili ya
mishahara.
Aidha Halmashauri imekisia kukusanya
Jumla ya Tsh 5,114,157,735.00 toka vyanzo vya ndani ambayo fedha hii
imejumuishwa katika jumla ya Bajeti ya mwaka 2018/2019. Jumla ya Tsh.
3,030,016,641.00 sawa na 60% zimetengwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.
Akiongeza katika ukumbi wa Halmashauri
ya Mji Geita kwenye kikoa cha kupitisha bajeti ya Mwaka wa
fedha 2018/2019,Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa
Geita,Mhandisi Modest Aporinali alisema Bajeti hyo imezingatia vipaumbele
vilivyoainishwa kwenye Mwongozo wa kuandaa Bajeti uliotolewa na Wizara ya Fedha
Mwezi, Novemba 2016, Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs 2030); Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020, Mpango wa Pili wa miaka Mitano (FDYPII)
2016/17-2020/21 na Lengo likiwa ni kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo
2030.
“Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa
Fedha 2018/2019,kwenye halmashauri hiyo kuwa imejielekeza katika
kufikia vipaumbele vyenye shabaha na
malengo yafuatayo Kuendelea kuboresha na kuimarisha
mfumo wa makusanyo ya mapato ya ndani ili kuongeza mapato ya Halmashauri. Kuboresha Sekta za huduma za jamii, hususan, Elimu,
Afya, Maji,Barabara, Mifugo, Uvuvi, Kilimo, Misitu, Maendeleo ya
Jamii, Ushirika.Kusaidi Sera ya Taifa kufikia Uchumi wa kati wa uendelezaji wa
viwanda.Kuimarisha Utawala bora”Alisema Modest
Aidha ameongeza kuwa Halmashauri inategemea kukusanya mapato yake kutoka kwenye vyanzo
mbalimbali kama kodi ya huduma( service levy) kutoka kampuni ya Mgodi wa
Dhahabu Geita na Kampuni nyingine zinazofanya kazi na Mgodi huo, kodi ya nyumba
za kulala wageni, Leseni za biashara,faini mbalimbali, upigaji chapa mifugo na
ushuru wa mifugo, ushuru wa mazao mbalimbali na matunda.
“Katika Bajeti ya mwaka 2018/2019. Jumla ya Shilingi
15,585,248,344 zimetengwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo, Kiasi cha shilingi
24,632,539,165 kwa ajili ya mishahara ya watumishi na Shilingi 4,765,976,688
kwa ajili ya matumizi mengineyo”. Aliongeza Mhandisi Aporinaly
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Geita Mheshimiwa Leonard Kiganga
Bugomola alisema kwa mwaka wa fedha uliopita Halmashauri ilipanga
kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 5, ambapo hadi kufikia mwezi Disemba 2017
Halmashauri imeweza kukusanya kiasi cha Shilingi 2,868,353,850.15 sawa na asilimia
52.
Mh. Bugomola ameongeza kuwa kutokana na mafanikio ya ukusanyaji uliofikia
nusu ya makadirio ana imani kuwa mpaka kukamilisha mwaka wa fedha 2017/2018
mwezi Juni mwaka huu, Halmashauri itakuwa imefikisha lengo la makusanyo. Aidha
makusanyo hayo yanatoa mwanga wa mafanikio katika bajeti iliyopitishwa
kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo,Mwl Herman
Kapufi amewasisitiza wajumbe kuwa na ukusanyaji mzuri wa mapato hili
kuweza kutekeleza bajeti kwa uzuri zaidi.
Katika Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019, Halmashauri ya Mji
Geita imejielekeza katika kufikia vipaumbele vyenye shabaha na malengo ambayo
ni Kuendelea kuboresha na kuimarisha mfumo wa makusanyo ya mapato ya ndani ili
kuongeza mapato ya Halmashauri, Kuboresha Sekta za huduma za jamii,
hususan, Elimu, Afya, Maji, Barabara, Mifugo, Uvuvi, Kilimo, Misitu, Maendeleo
ya Jamii, Ushirika,
Kusaidia Sera ya Taifa kufikia Uchumi wa kati wa uendelezaji wa viwanda
na Kuimarisha Utawala bora.
No comments:
Post a Comment