|
Baadhi ya wanafunzi shule ya Msingi ya Uyovu wakiwa kwenye sherehe za kutimiza miaka Kumi tangu kuanzishwa kwa shule Hiyo |
|
Mgeni rasimi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bukombe pamoja na msafara wakiingia kwenye viwanja vya maazimisho ya sherehe za jubilee yaliyokuwa yakifanyika kwenye viwanja vya shule Hiyo pembeni yake mkono wa kushoto ni mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Nicas Safari. |
|
Msafara ukiingia kwenye viwanja shughuli inapofanyika. |
|
Kwaya ya wanafunzi shuleni hapo ikiingia kutoa Burudani ya uwimbaji. |
|
Wadau mbali mbali wakiwemo walimu pamoja na wazazi wakifuatilia kwa makini shughuli ya uwimbaji iliyokuwa ikiendelea. |
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ,Nicas Safari Mayala akijitambulisha mbele ya wanafunzi na wazazi ambao walikuwa wamefika kwenye sherehe Hizo. |
|
Wanafunzi wa Skauti wakionesha ukakamavu wao kwa kutengeneza mnara kwenda Juu kwa kubebana wao kwa wao. |
|
Skauti wakivunja Tofari lililokuwa tumboni kwa mwanaskauti. |
|
Mwalimu Mkuu wa Shule y Sekondari Uyovu, Saimon Mashauri akielezea mbele ya mgeni Rasmi Makusudi na Malengo ya kuwepo kwa sherehe ya Jubilee ya Miaka Kumi tangu kuanzishwa kwa shule hiyo. |
|
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Uyovu Josephat Waka akielezea changamoto za watoto kukatishwa masomo kutokana na kupigwa mimba wakiwa katika kipindi cha umri mdogo. |
|
Meza Kuu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe pamoja na Mbunge na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo. |
|
Vijana wa Kudesi na Kubugi wakionesha mautundu yao wakati wa sherehe ya miaka kumi ya shule ya Sekondari ya Uyovu. |
|
Mbunge wa Jimbo Bukombe Dotto Biteko,Akitoa neno la utangulizi na kumkaribisha Mgenu Rasmi kwaajili ya kuzungumza na wazazi wanafunzi na baadhi ya wananchi waliuzulia Hafra hiyo. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga akizungumza na wananchi waliofika kwenye Hafra Hiyo ambapo moja kati ya maagizo ambayo ameyatoa ni watuhumiwa kukamatwa ndani ya wiki inayokuja. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe hakigawa vyeti vya pongezi kwa idara ambazo zimefanya vizuri shuleni hapo. |
Wanafunzi 11
wote wakiwa wa Sekondari,sita kutoka Uyovu Wilayani Bukombe Mkoani
Geita,wamekatishwa masomo yao baada ya kupata ujauzito huku baadhi ya watendaji
wa Serikali Idara ya Elimu Wilayani humo wakidaiwa kugeuza mtaji matukio hayo kwa
kushirikiana na wazazi,wanaume waliowapa mimba kisha kuyamaliza kimyakimya.
Hayo
yamebainishwa na Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Uyovu Josephat Waka
ambaye ameibua tuhuma hizo mbele ya viongozi mbalimbali wa chama na
Serikali akiwemo mkuu wa Wilaya hiyo na
Mbunge wa jimbo hilo wakati wa Jubilee
ya miaka kumi tangu ilipoanzishwa shule hiyo.
“Hadi
kipindi hiki kuna mimba sita kwenye shule ya sekondari ya uyovu sisi kama bodi
tumejitaidi kupeleka taarifa sehemu husika lakini taarifa ya kusikitisha kuna
baadhi ya wazazi watumishi sio waaminifu wamekuwa wakishirikiana na watu hawa ambao wamewapa watoto mimba mwisho
wa siku wanatoroka mimi kama mwenyekiti wa Bodi nilikuwa nimefikilia Jambo moja
endapo kama tutawapata chama cha wanasheria wanawake kuja na kutusaidia swala
hili naamini tutamaliza tatizo hili maana linasumbua kwa kiasi kikubwa katika
maeneo yetu”Alisema Waka.
Hata Hivyo
Mwenyekiti wa Bodi ya shule ameongezea kuwa Jitihada ambazo wamekwisha
kuzichukua hadi sasa ni kwamba wanampango wa kukaa na wazazi waweze kuchangia
ujenzi wa hostel ambazo zinatasaidia kunusuru Mimba za watoto wa kike katika
shule.
“Ndugu
mwandishi najua kuwa hapa uyovu ni eneo la biashara na mala nyingi kuna mabinti
ambao wanaishi mbali na maeneo haya kwa hiyo unakuta wanapanga kwenye makazi ya
watu mwisho wa siku wanapopata shida wanarubunika na kujikuta wakiingia kwenye
mchezo wa mapenzi hivyo jitihada kubwa tunaona sisi kama Bodi ya shule ni
kukutana na wazazi na kuwaomba kuchangia ili tuweze kujenga hostel kwa kushirikiana
na serikali”Alisema Waka
Mbunge wa
Jimbo hilo Dotto Biteko ambaye alikuwa ameambatana na Mgeni Rasmi ambaye ni
Mkuu wa Wilaya Hiyo,amesikitishwa na taarifa hizo ambapo amechukua nafasi hiyo
kuwahasa wanafunzi kuachana na tabia ya kuharakia mapenzi katika umri mdogo.
“Tumeambiwa
hapa kuna mimba sita kwenye shule hii Mh Mkuu wa Wilaya Nitashangaa sana endapo
kama kuna mtu amemtia mimba mwanafunzi
yupo mitaani hajachukuliwa hatua zozote za kisheria kama kuna mzazi ambaye
mtoto wake amepatwa mimba na anakwenda kuonga ili Yule aliyemtia mimba mtoto
wake aachiwe huru mimi inaniuma sana unakuta mtoto mdogo ametiwa mimba
anaangaika na mtoto lakini mwanaume yeye anaendelea na maisha yake bila shida
yoyote ,Nanyinyi wanafunzi tunawaomba msome sio uko shule na wewe unakuwa na
maswala ya Bebi subilia wakati wako utafika”Alisisitiza Dotto.
Kaimu Afisa
elimu wa Wilaya hiyo Mwl Leornad Kingwa mbali
na kukiri wanafunzi sita wa Sekondari hiyo kukatishwa masomo kwa ujauzito
wamedai wamekwishaanza kuchukua hatua huku mkuu wa Wilaya hiyo Maganga akiagiza
kufikia wiki ijayo awe amepewa orodha ya majina ya wanaume waliowapa mimba
watoto hao ili achukuwe hatua haraka iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na
kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria.
“Changamoto
zipo wajawazito wapo wanapatikana kiwilaya wanafunzi takribani kumi na moja
wanaujauzito ingawa shule ya uyovu ndio imeonekana kuwa na wanafunzi wengi
zaidi tumeshachukua hatuia taarifa zipo kwenye jeshi la polisi tayario”Alisema
Kingwa.
Hata hivyo
baadhi ya wazazi Julius John na Lucy Malaki pamoja na kumshukuru Mkuu wa wilaya
kwa maamuzi ambayo ameyachukua pia wamewaomba watu wenye tabia za kuwakatisha
masomo mabinti waliopo mashuleni kuachana na Tabia hiyo kwani imekuwa ikisababisha kudidimiza ndoto za
wasichana wengi..
No comments:
Post a Comment