Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia Bungeni leo
kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya Mapato na
matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wito kwa waajiri na
waajiriwa wote nchini kuzingatia Sheria za kazi na kuimarisha uhusiano katika
kazi ili kutumia muda mwingi kufanya kazi badala ya kutatua migogoro kazini.
Ameyasema hayo
alipokuwa akitoa hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na
makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha
2017/2018.
“Niwaombe waajiri na
waajiriwa kuzingatia Sheria za kazi tupunguze migogoro kazini ili tuweze
kuendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kufanya kazi” alisisitiza Mhe.
Majaliwa.
Ameongeza kuwa
Serikali imefanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 58 ya migogoro ya kikazi
inatokana na kutozingatiwa kwa taratibu za kuachishwa kazi kwa waajiriwa.
Amezitaja Sekta
zinazoongoza kwa migogoro ya kazi kuwa ni
Usafirishaji,ujenzi,ulinzi,binafsi,elimu,huduma za Hotel na Viwanda.
Katika kupunguza
migogoro mahali pa kazi Serikali imefanya kaguzi na kusimamia uundwaji wa
Mabaraza ya Wafanyakazi na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi imeendelea kutimiza
wajibu wake wa kusuluhisha migogoro ambapo katika kipindi cha Julai hadi
Februari 2016 jumla ya migogoro 8,832 ilisajiliwa na kati ya hiyo
migogoro 3,319 sawa na asilimia 37.6 ya migogoro iliyosajiliwa imesuluhishwa.
No comments:
Post a Comment