Madarasa ambayo yapo kwenye shule ya Msingi Kambarage 14 yakionekana kukamilika kwa nje. |
Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi CCM Kata ya Buhala hala ikikagua mradi huo katika utekelezaji wa Ilani ya chama hicho. |
Daud Benson Ambaye ni Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Buhala hala akielezea namna ambavyo wamerihishwa na shughuli ambazo zimefanywa na serikali kwa ushirikiano wa Diwani wa Kata Hiyo |
Daud Benson Ambaye ni Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Buhala hala akimsisitiza Diwani wa kata hiyo Mussa Kabese kufanya kazi kwa bidii za wananchi ili kutimiza ilani ya chama hicho. |
Mwenyekiti wa kata ya Buhala hala,Fanuel Emmanuel akielezea matarajio ya kuona shughuli za maendeleo zinatekelezwa kwa wakati Katika kata Hiyo |
Diwani wa Kata ya Buha hala ,Mussa Kabese Akionesha maeneo ambayo ni ya mipaka ya shule hiyo kwa Kamati ya Siasa kwenye kata Hiyo. |
Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rasi
Dk John Magufuli imeendelea kutekeleza ahadi zake za utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa shule za msingi Kwenye mitaa na Kata Tofauti ndani ya halmashauri
ya Mji wa Geita Wilayani humo, ikiwa ni juhudi za kuondoa usumbufu wa wanafunzi
kutembea umbali wa kilomita ndefu .
Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi
CCM Kata ya Buhala hala Imetembelea
mradi unaoendelea katika Mtaa wa 14 kambarage,
wakitimiza matakwa ya kikatiba
ndani ya chama hicho ambayo inawataka viongozi kutembelea na kujionea
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kama ambavyo ibara ya 189 ya mwaka 2015/20
inavyosema.
Akizungumza na wajumbe waliotembelea
shule hiyo mpya ambayo iko mbioni kukamilika Diwani wa kata ya Buhala hala Musa Kabese
amesema kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha sh Milioni mia moja (100) na kwamba
walitakiwa wajenge majengo matatu lakini wao wamekwenda mbele zaidi na kujenga
madarasa manne.
“Wajumbe kama mnavyoona haya ni
madarasa manne ambapo ujenzi huu umegharimu kiasi cha Sh,milioni Mia moja
tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumevuka malengo tuliambiwa madarasa matatu lakini
sisi tumekwenda mbele tumejenga manne.”Alisema Kabese
Mwenyekiti wa CCM kata ya Buhalahala
Fanuel Emmanuel alisema moja kati ya majukumu ya chama cha mapinduzi CCM ni
kutekeleza ilani yake na kwamba kwa sasa uchaguzi umekwisha kumalizika ni vyema
kazi zikafanyika na zikaonekana kutokana na ahadi ambazo walizitoa wakati wa
kampeni kwa wananchi.
Nao baadhi ya wajumbe wamesema shule
hiyo itakapokamilika na kuanza kutumika itaondoa kero ya wanafunzi kutembea
umbali mrefu, huku wakibainisha maeneo ambayo bado yanakabiliwa na changamoto.
No comments:
Post a Comment