Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Elisha Lupuga akisoma maadhimio ya Baraza Juu ya kuwasimamisha Watumishi wawili ambao wamekiuka misingi ya ajira. |
Diwani wa Kata ya Nyamalimbe Jeremia Ikangala Akiunga Mkono maadhimio ya baraza la madiwani la kuwafukuza kazi watumishi na kuwasimamisha watumishi wengine kwaajili ya kupisha uchunguzi. |
Baadhi ya madiwani wakifuatilia kikao maadhimio ya Baraza hilo. |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ,Ali Kidwaka akisikiliza maadhimio ambayo yalikuwa yakitolewa na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo. |
Baraza la
Madiwani halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani humo kupitia mamlaka ya nidhamu
ya watumishi imewafukuza kazi watumishi wawili wa halmashauri hiyo kwa utovu wa
nidhamu na utoro kazini kwa muda mrefu. Na kuwasimamisha kazi watumishi wengine
wawili kwa lengo la kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili.
Akitanganza
uamuzi huo mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Elisha Lupuga, baada ya baraza hilo
kujiegeuza kuwa kamati ya nidhamu kwa
dharula amesema hatua hiyo ni kuonesha
namna gani watumishi wanatakiwa kufuata nidhamu kazini.
Mwenyekiti
huyo amewataja waliofukuzwa kazi kuwa ni Nzalagaza Nyanda ambaye alikuwa
idara ya utawala na Alphonce Mgimwa ambae alikuwa ni muuguzi katika
zahanati ya Furu ambae aliondoka kazini
siku 50 bila taarifa .
Waliosimamishwa
kwaajili ya uchunguzi ni mhandisi wa maji Halmashauri hiyo Rahel Antony ambae
amesimamishwa kwaajili ya kupisha uchunguzi wa mradi wa maji wa Chankorongo
ambao umesuasua kutokumalizika kwa miaka mingi na Denis Nyasaba ambae ni afisa
ugavi wa halmashauri ambaye anachunguzwa kwa mikataba mibovu ya miradi.
“Kwa mujibu
wa sheria za kanuni ya arobaini na mbili jedwali la kwanza sehemu A kipengele
cha nne cha kanuni za utumishi wa uma za
mwaka 2003 na kanuni ya 57 kifungu kidogo cha kwanza cha kanuni za utumishi wa uma ambapo namba F
16 kifungu kidogo cha kudumu cha mwaka 2009 watumishi hawa kuwa watoro kazini
na kwamba wanaposhindwa kufika ofisini ndani ya siku tano sheria inatambua
kuwafukuza kazi kwa hiyo natangaza kuanzia leo watumishi hawa wamefukuzwa kazi kwa kuzingatia mamlaka
ya kazi za uma “Alisisitiza Lupuga.
Madiwani wa Kataza
Bukondo na Lwamgasa John Maguru na Dotto
Kaparatus amepongeza hatua hiyo huku wakiwataka watumishi kufuata kanuni na
taratibu za mikataba ya ajira na pia kuwa waaminifu pindi wanapopatiwa kazi.
IMEANDALIWA
No comments:
Post a Comment