Hofu imetanda kwa wananchi wa kitongoji cha Sikalibuga
kijiji cha Businda kata ya Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita kwa
kuongozwa na wenyeviti wawili katika
kitongoji kimoja kinyume na
sheria.
Hatua hiyo imekuja mara
baada ya serikali wilayani humo kumuondoa aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji
hicho toka mwaka 2015 kwa sababu mbalimbali zinazo eleza kuwa ni
matumizi mabaya ya madaraka.
Akizungumza katani hapo
Diwani wa kata hiyo ya Ushilombo Bw. Lameck Warangi amemtaja mwenyekiti aliyeondolewa
katika kiti cha uongozi tangu mwaka 2015 kuwa ni Malisera John mkazi wa Sikalibuga.
Bw. Warangi amesema
chanzo kilichosababisha kiongozi huyo kuondolewa ni pamoja na kutuhumiwa kwa makosa matatu
ambayo ni kuuza eneo la kijiji bila kufuata uataratibu wa kisheria,matumizi
mabaya ya madaraka na kushindwa kuitisha mikutano ya hadhara kisheria tangu alipo chaguliwa .
Kwa upande wa kaimu
mwenyekiti aliye chaguliwa na wananchi katika eneo hilo Bw. Mandago Singu
ameelaza kuwa amekutana na changamoto nyingi tangu achaguliwe kukaimu kitongoji
hicho kwani mwenyeki wa aliyekuwepo amegushi nyaraka za serikali ikiwa ni
pamoja na kuchonga mhuri feki na amekuwa
akifanya kazi kama mwenyekiti haliyakuwa
ameondolewa kisheria .
Sambamba na hilo Bw. Singu
ameiomba serikali yenye dhamana ya kulishughulikia jambo hilo ifanye haraka
iwezekanavyo ili kuepuka matatizo yasiyo kuwa yalazima ambayo yanaweza
kujitokeza kijijini humo.
No comments:
Post a Comment