Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Mponjoli Mwabulambo akizungumza na waandishi juu ya tukio la mtoto aliyeuwawa. |
Bi,Elizabeth Selemani ambaye ni mama wa mtoto aliyefanyiwa ukatili akielezea mazingira ya mtoto wake kufanyiwa kitendo hicho. |
Mtoto wa
umri wa mwaka mmoja na miezi saba ambaye ambaye jina lake tumelihifadhi kwa ameuwawa
kikatili na kuchomwa na moto sehemu za
makalio.
Tukio hilo
limetokea katika kijiji cha Nyalubanga ,kata ya Lwezera Wilaya na Mkoa wa Geita
, ambapo anayesadikika kufanya tukio
hilo ni Baba wa Kambo anayejulikana kwa jina la Petro Bahati(35).msukuma
mkazi wa kijiji hicho.
Akizungumzia
tukio hilo Mama mzazi wa mtoto aliyefariki Bi,Elizabeth Selemani ameelezea kuwa
wakati tukio hilo linatokea yeye alikuwa Bafuni akioga na mtoto alimuacha mume
wake akiwa na mtoto ambaye ni marehemu kwa sasa .
Bi,Elizabeth
ameendelea kueleza kuwa alipokuwa akikoga alikuja mume wake akiwa na hasira na
kumwomba kanda mbili kuwa hampatie ili haondoke mala baada ya kupatiwa
aliondoka huku akimwacha bafuni na kuelekea kusiko julakana na baadae aliporudi
ndani alimkuta mtoto akiwa amekalishwa alipomsogelea alimkuta akiwa na majeraha
sehemu za shingoni na kwenye makalio akiwa amechomwa moto hali ambayo
ilimpelekea kutoa taarifa kwa majirani.
“Nilikuwa
ninaishi nae vizuri tu wala hakuwa na tatizo kwa mtoto sijui ni nini ambacho
kimempata hadi kufikia hatua hii yani hata na mimi nimechanganyikiwa kwakweli”Alisema
Elizabeth.
Kamishina
Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita ,Mponjoli Mwabulambo amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa wa tukio hilo hajakamatwa na
wanaendelea na juhudi za kumtafuta ili aweze kufikishwa kwenye Mkono wa sheria.
Na kwamba tukio hilo ni la pili kwa maeneo hayo.
Huku akitoa
rai kwa wananchi wanaojihusisha na vitendo vya kikatili kama vya namna hiyo
kuacha mara moja kwani jeshi hilo alitasita kuchukua hatua kari za kisheria
dhidi ya vitendo hivyo.
Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Geita,ambaye pia ni mkuu wa wilaya Mwl
Herman Kapufi amechukua nafasi hiyo kuwahasa wanananchi hususani ni wasichana na wanawake kuwa
waangalifu pindi wanapotaka kuolewa na watu wasio wajua.
No comments:
Post a Comment