Waziri wa Habari,
Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Dkt. Harrison George Mwakyembe
akisalimiana na waalimu na viongozi wa Chuo cha Waalimu wa Michezo Malya Jijini
Mwanza alipofanya ziara ya kikazi na kushiriki mahafali ya Chuo hicho na kutoa
vyeti kwa wahitimu.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Dkt Harrison George Mwakyembe
akizungumza katika mahafali ya Chuo cha waalimu Michezo Malya Jijini Mwanza.
Mmoja wa wanafunzi
wahitimu katika Chuo cha Waalimu wa Michezo Malya Jijini mwanza akisoma risala
kwa niaba ya wanafunzi wenzake katika mahafali ya chuo hicho.
Mkurugenzi wa Michezo nchini Bw. Yusufu Omary Singo akitoa nasaha kwa
wahitimu wa mafunzo katika mahafali ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa
kozi fupi ya uwalimu wa michezo yaliyofanyika Chuo cha Mwaalimu wa Michezo
Malya Jijini Mwanza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Harrison
George Mwakyembe akitoa cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kozi fupi ya uwalimu wa
Michezo katika Chuo cha waalimu wa Michezo Malya Jijini Mwanza.
Baadhi ya wanafunzi na wahitimu wa kozi fupi ya uwaalimu wa michezo
wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Dkt.
Harrison George Mwakyembe alipokuwa akizungumza nao katika mahafali ya Chuo
hicho Jijini Mwanza.
Serikali imesema itakuwa
bega kwa bega na Chuo cha michezo Malya ili kuhakikisha chuo hicho kinakuwa
kitovu cha kuzalisha walimu bora na wenye weledi katika masuala mazima ya
michezo hapa nchini na hata nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na
Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Harrison George
Mwakyembe, alipokuwa akifunga mafuzo ya muda mfupi yanayo tolewa na chuo hicho,
ambapo jumla ya wahitimu wapatao sitini na tisa (69) walitunukiwa vyeti na
waziri huyo.
Mwakyembe amesema, kama
wizara, nilazima wakifanye chuo cha Michezo Malya kuwa “Strategic thinking” kwa
maana ya stratejia ya wavumbuzi wa vipaji vya watu wa kada mbali mbali hususan
katika suala zima la walimu wa michezo “Nilipo tembelea na kukiona chuo
nimepata picha kamili ya chuo hiki, hii sasa inanipa shauku yakuwashauri
muandae dira endelevu kwa chuo chetu” alisema Mwakyembe.
Mwakyembe, amesema
katika Ibara ya 161 (G) ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2015-2020, inaweka
bayana na kutia msukumo wa masuala ya michezo, lakini pia Rais wa Jamhuri ya
Muungano ameonesha dhamira ya dhati katika hilo hata mbele ya Mataifa mengine
ndio sababu Morocco, wanataka kujenga ‘Sport Complex’ Makao Makuu ya nchi
Dodoma.
Kwa upande wake Mkuu wa
chuo hicho, amesema katika kuhakikisha chuo hicho kinafanya vema katika siku za
usoni wamedhamiria kuongeza idadi ya kozi zitakazo kuwa inatolewa kwa
wakurufunzi wanaotaka kujiunga na chuo hicho ukiwepo mchezo wa Whushu ambapo
China kupitia ujumbe wake iliowakilishwa na Bi. Amber, uliozulu chuoni hapo
wakati wa mahafali, umeonesha nia yakuleta walimu wa Whushu.
Mbali na jukumu la
kuongeza aina ya kozi zitakazo tolewa na chuo hicho kwa ngazi ya Stashahada
(Diploma) mkuu huyo amemweleza waziri changamoto zinazo kikabili chuo hicho
ambazo nipamoja na uhaba wa maji, Gym ya mazoezi, hali inayosababisha timu
mbali mbali za mpira wa miguu zinazo tamani kwenda kuweka kambi katika eneo
hilo kushindwa kutokana na ukosefu wa Gym, “Mh. Waziri ilikuja timu ya Mbao FC,
kilio chao kikubwa ilikuwa ni eneo la Mazoezi ya viungo (Gym Fitness
centre)” alisema mkuu huyo wa chuo.
Katika hatua nyingine
Mkurugenzi wa Michezo nchini Dkt. Yusuph Singo Omary, kutoka Wizara ya habari,
amesema hivi sasa Serikali ipo katika mchakato wa kutenga shule 55 ikiwa ni
hatua itakayo saidia katika kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo nchini
kuanzia vijana wanapokuwa wadogo.
Awali akimkaribisha
Waziri wa habarikuzungumza katika mahafali hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba,
Mhandisi Mtemi Msafiri, alimuomba waziri, Wizara ya habari kwa kushirikiana na
Wizara ya Elimu na TAMISEMI, kuona Umuhimu wakukisaidia chuo hicho katika
kukiendeleza, “Tunaomba Mhe. Waziri ili chuo hiki kiweze kwenda mbele basi vema
kila Halmashauri ikaagizwa kugharamia angalau Walimu wawili kila mwaka”,
alisema Msafiri na kuongeza kuwa endapo Halmashauri zote nchini 189, zikileta walimu
wawili tu basi tutakuwa na wanafunzi 378, hii itakisaidia chuo chetu kukua
zaidi, lakini pia kupata walimu wenye weledi.
Kwa upande wao wahitimu
hao wamemuomba waziri ku
pewa kipaumbele katika Michezo ya UMISETA na
UMITASHUMTA, Akisoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Catherine Laurent,
amesema wao wamejifunza Sheria na kanuni za Michezo mbali mbali kwa kipindi
chote walichokuwepo chuoni hapo hivyo wanaomba kupewa kipaumbele katika
kufundisha michezo pindi warejeapo kwenye vituo vyao vya kazi kwani sasa
wanatambua sheria, kanuni na taratibu zinazo ongoza michezo waliyo jifunza.
Chuo cha michezo Malya
kilianzishwa mwaka 1979, kikiwa na lengo la kufundisha na uendeleza walimu wa
michezo katika ngazi ya Astashahada na badae mwaka 1995, ndipo kilianza kuzalisha
walimu wanafunzi wa ngazi ya Stashahada (Diploma). Lakini pia kimekuwa
kikiendesha kozi fupi za wiki mbili ambazo huwajengea uwezo wahusika kabla
yakuendelea na ngazi ya Diploma.
No comments:
Post a Comment