Monday 24 April 2017

BAADHI YA WAKAZI WA BUKOMBE MKOANI GEITA WAKWERWA NA UTUNZAJI HAFIFU WA MIFUGO



Baadhi ya wananchi wilayani Bukombe mkoani Geita wameiomba serikali kusimamia sheria za mifugo ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mifugo hiyo kuzurula katika makazi yao na kuwasababishia hasara kubwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi yao wamesema kuwa mifugo hiyo imekuwa kero kwao kutokana na wamiliki wa mifugo kuiachia ovyo na kusababisha  uharibifu wa mazao yao pamoja na bustani za mboga mboga na matunda.

Bw. Erasto James Katambi na Bi. Magret Seleman wameitaja mifugo hiyo  kuwa ni pamoja na mbuzi, kondoo, punda, nguruwe, mbwa na kondoo na kuiomba Serikali kuwaelimisha wafugaji wa mifugo inayozurula ovyo ili kuepuka kuendelea kuwa kero kwa wananchi.


Naye afisa mtendaji wa kata ya Igulwa wilayani Bukombe Bi. Gaudensia Dalaali amekiri kuwepo kwa kero hiyo na amewataka wafugaji kufuga mifugo yao kwa kufuata sheria na taratibu kwani bila kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya atakayekutwa na hatia.

No comments:

Post a Comment