Mfadhili wa timu ya Buselesele FC ,Godfrey Miti akifuatilia Mchezo wa TOTO na Buselesele FC ambapo ilikuwa ni mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye viwanja vya shule ya sekonadari ya Buselesele. |
Mashambulizi yakiendelea kwa timu zote mbili. |
Mashabiki wakifuatilia mtonange huo. |
Benchi la Toto afrikani baadhi ya wachezaji wakicheki mchezo. |
Kocha Mkuu wa timu ya Toto African ya Jijini Mwanza maarufu
wanakisha mapanda, Furgence Novatus
amesema timu hiyo kamwe haitashuka daraja kutokana na matumaini makubwa ya ushindi kwa
mechi nne walizobakiza licha ya kuwa
wako katika mstali wa hatari kushuka ligi.
Kocha huyo
ametoa tambo zake mara baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki kati ya Toto
African na Buselesele FC, mabingwa wapya wa Mkoa wa Geita ligi daraja la tatu,
ambapo Novatus amesema hata Mabingwa wa ligi kuu timu ya Yanga hawatawabakisha
salama wasipojipanga na kwamba hakuna urafiki katika hatua waliopo.
Baada ya
mchezo huo ambao timu hizo zilitoshana nguvu, wadau wa soka Mkoani Geita
wamekuwa na matumaini makubwa na timu yao, ambayo iko katika maandalizi ya
kuchuana ligi daraja la pili.
Diwani wa
kata ya Buselesele Godfrey Miti ambaye ni mdhamini wa Timu ya Buselesele FC
amedai kuwa matumaini makubwa aliyonayo ni kuakikisha timu hiyo inafikia
kiwango cha ligi kuu na kwamba yeye pamoja na wadau wa mpira Mkoani Geita
hataakikisha timu hiyo inapanda daraja.
No comments:
Post a Comment