Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella
Kairuki akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano
wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Serikali imewasahuri
wananchi wote wanaofaidika na Mpango wa kunusuru Kaya Maskini (TASAF) nchini
kuzitumia vizuri ruzuku wanazozipata kwa kuendelea kujishughulisha na shughuli
za kiuchumi katika maeneo yao.
Akijibu swali la
Mbunge wa Mtabwe Mhe. Khalifa Mohamed Issa lililouliza Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii (TASAF) upo katika Awamu ya Tatu ya Utekelezaji wa Mpango wa kunusuru
Kaya Maskini nini kimefanyika ili ruzuku ziweze kumudu mahitaji ya chakula,
Elimu, Afya na lishe Bora kwa watoto.
Waziri wa Nchi ofisi
ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amesema kuwa Serikali
inaendelea kutoa ruzuku wa Kaya Maskini ila inasahuri pia wananchi waendelee
kujishughulisha na kazi nyingine za kuongeza kipato na isitegemee ruzuku pekee.
“Niwaombe wananchi
wanaopata ruzuku kutoka mpango wa TASAF wajishughulishe pia na shughuli
nyingine za kiuchumi na kutotegemea ruzuku pekee” Alisistiza Mhe. Angella.
Ameongeza kuwa ruzuku
zinazotolewa ni kichocheo cha kuifanya kaya iweze kujikimu hasa katika kupata
mahitaji muhimu huku ikiendelea kujiimarisha kiuchumi kwa kuweka akiba na
kutekeleza miradi ya ujasiriamali ili iweze kusimama yenyewe na kujitegemea
baada ya kutoka katika umaskini uliokithiri.
Mhe. Angella Kairuki
ameeleza kuwa vigezo vya kupata kaya maskini ni wa uwazi na huanishwa na Jamii
katika mkutano wa hadhara unaoendeshwa na wawezeshaji kutoka Halmashauri za
Wilaya na kusimamiwa na Viongozi wa Vijiji, Mitaa na Shehia.
Aidha uzoefu
uliopatikana umeonesha kwamba kwa kiwango cha ruzuku kinachotolewa kwa wananchi
wanaofaidika na Mpango huo kimewawezesha kuboresha maisha yao kwa kufanya
shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo ufugaji,ujasiriamali na ujenzi
wa nyumba bora, hivyo viwango hivyo sio vidogo kama wengi wanavyodhani.
No comments:
Post a Comment