Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwasili kwenye ofisi za Kijiji cha Katandalo.hapa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa kijiji hicho. |
Mkuu wa wilaya akisaini kwenye kitabu cha wageni Kijiji cha Katandalo. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwasisitiza wananchi kulima kilimo ambacho kitaleta manufaa kwao. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akikagua shamba la Mihogo |
Mkuu wa wilaya ya Geita akikagua shamba la pamba |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimpongeza mkulima wa pamba ambaye alipendezwa na maendeleo ya shamba lake. |
Mkuu wa
wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi amewataka maafisa kilimo na umwagiliaji
kufanya tathmini halisi ya mazao yanayoweza
kustawi kwenye maeneo tofauti na mazao watakayobaini kuwa yanastawi vizuri
wawahimize wananchi kuyalima
Mwl Kapufi
amesema hayo wakati akiwa kwenye zoezi la kukagua mashamba ya pamba ,mtama na
Mihogo kwenye Kata ya Kaseme na Magenge Wilayani Humo.
Amesema kuwa
kutokana na mabadiliko ya Hali ya Hewa ni vema maafisa kilimo wakatembelea
maeneo na kuangalia aina ya mazao
yanayostawi
“Kwa wilaya yetu ya Geita Halmashauri ya
Wilaya na Halmashauri ya Mji natoa wito kwanza kwa maafisa kilimo na
umwagiliaji wote waweze kufanya tathmini halisi ya mazao ambayo yanatakiwa
kustawi katika eneo husika, hayo mazao ambayo yatastawi kwenye maeneo hayo ndiyo
tuwahimize wananchi waweze kulima kwenye maeneo hayo”Alisema Kapufi.
Hata hivyo
wakulima wa zao la pamba katika kijiji
cha Katangalo kata ya Kaseme wamemwambia Mkuu wa wilaya kuwa kukosekana kwa
pampu za kutosha kwa ajili ya kunyunyuzia dawa kunasababisha uharibifu
mkubwa wa zao hilo la kibishara kwani
kwa sasa wakulima takribani 300 wanatumia pampu moja ambayo haitoishi kwa
mahitaji yao.
Akijibu kero
hizo Mkuu wa Wilaya Mwalimu Herman Kapufi, amewataka watendaji wa serikali za vitongoji na Vijiji kuwa na mfumo mzuri wa
kubainisha changamoto za wakulima ili zipatiwe ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment