Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt. Medard Kalemani akijibu hoja
mbalimbali za wabunge katika kikao cha pili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11
Mjini Dodoma.
Hilo limebainishwa na
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt. Medard Kalemani alipokuwa
akijibu swali la Mbunge wa Newala Mjini Mhe. Kepteni Mstaafu George Huruma
Mkuchika lililouliza “Serikali iliwaahidi wananchi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara
umeme wa uhakika na wa kutosha baada ya kugundulika kwa Gesi lakini bado
kumekuwa na tatizo la kukatika kwa umeme?.
Mhe. Dkt. Medard
Kalemani ameeleza kuwa katika kuondokana na tatizo hilo Serikali inafanya
ukarabati wa Mtambo ulioharibika ili kurudisha uwezo wa kituo katika hali yake
ya kawaida ya kuzalisha MW 18.
“ Nia ya Serikali ni
kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya Umeme kwa asilimia kubwa hasa kwa
wale waishio vijijini” alisisitiza Mhe. Kalemani.
Ameongeza kuwa katika
kuendeleza juhudi za upatikanaji wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara
imeongezewa mitambo sita (6) yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa jumla ya MW 12
kama hatua ya muda mfupi.
Aidha katika kuboresha
hali ya upatikanaji endelevu wa umeme katika Mikoa hiyo, TANESCO inajenga njia
ya kusafirishia umeme yenye msongo wa kilovoti 132 yenye urefu wa kilomita 80
kutoka Mtwara hadi Mnazi mmoja Lindi.
No comments:
Post a Comment