Wednesday, 5 April 2017

JUMUHIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA GEITA YAADHIMISHA MIAKA 62 KWA KUWAONA WAGONJWA NA KUTOA MISAADA KWA WAITAJI.


Mwenyekiti wa Jumuhiyo hiyo Wilaya ya Geita,Ahamed Mbaraka Adam,akitoa pole kwa mama ambaye alikuwa amelazwa kwenye Kituo cha afya cha Katoro wakati wa ziara ya kuwaona na kuwasalimia wagonjwa. 







Mwenyekiti wa Jumuhiyo hiyo Wilaya ya Geita,Ahamed Mbaraka Adam ,pamoja na wajumbe wa jumuhiya hiyo wakikagua sehemu ya shule ambayo imepandwa miti.





Jumuhiya ya wazazi  wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita,imeadhimisha siku hiyo kwa kufanya  usafi  kwenye kituo cha afya cha katoro na kuwaona wagonjwa kituoni hapo.

Akizungumzia dhamira kuu ya  maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Jumuhiyo hiyo Wilaya ya Geita,Ahamed Mbaraka Adam ,ameelezea kuwa wao wameamua kufanya shughuli za usafi na kuwa Julia hali wagonjwa ni kutokana na kuona umuhimu wa Mama katika jamii na ndio sababu ya wao kuzungukia  hodi za wakina mama na kutoa vitu ambavyo walikuwa wameandaa.

Hata Hivyo Mbaraka ameongezea kuwa katika Kituo hicho cha afya wamegundua madhahifu yaliyopo ikiwa ni pamoja na hodi za wakina mama pamoja na upungufu wa vitanda.

“Katoro inawafanya biashara wengi sana ebu waone aibu maana ni vyema wakaguswa walau kuchangia swala la vitanda kwani hili sio hadi serikali ifanye ni wao kuona mapungufu na kuyashughulikia mimi nimuombe diwani  wa Kata hii ya Katoro kuwashirikisha wafanyabiashara waweze kuchangia swala la afya”Alisisitiza Mbaraka.

Awali akielezea  changamoto ambazo wanakutana nazo mbele ya wajumbe wa jumuhiya ya wazazi Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Katoro,Peter Janga ,alisema kuwa kwa mwezi mmoja wamekuwa wakipata wakina mama mia tano (500)na wodi iliyopo kwa sasa ni finyu hali ambayo imekuwa ikisababisha wakina mama kulala wawili wawili kwenye vitanda .

“Kituo cha Katoro  ni kidogo kwa miundo mbinu lakini wananchi ambao wanakuja katika kituo hiki ni wengi na kwasasa hivi tunafanya upasuaji hapa hapa hali ambayo imepelekea hodi ya wazazi ambao wanaofanyiwa upasuaji kuwa kuwa wengi na vitanda vilivyopo kwa sasa ni vitano tu”Alisema Janga

Katibu wa umoja wa wazazi Wilaya ya Geita,Happy James amekiri kuziona changamoto hizo kwenye kituo hicho na kwamba wataakikisha wanafikisha changamoto hizo kwenye mamlaka usika  hili ziweze kutatuliwa  kwani wanajua namna ambavyo wanawake wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua hivyo ni vyema mazingira yao yakawa kwenye hali iliyo nzuri.

Katibu Happy,ameongeza kuwa ni vyema kwa wanachama wa jumuhiya hiyo kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nyadhifa mbali mbali ndani ya jumuhiya hiyo kwani  fomu ni bure huku akisisitiza kutofanya kampeni zozote na kuepukana na vitendo vya Rushwa .




No comments:

Post a Comment