Mwenyekiti wa watunza mazalio na
makulio ya samaki Bashiri Manampa
kutoka Mwaro wa Nyamilembe wilayani Chato mkoani Geita amewashukuru
wenyeviti wenzake wa miaro ya buhungu na nyakakarango kwa kufungua mipaka
ili kukomesha uvuvi haramu ndani ya ziwa victoria.
Akizungumza ofisini kwake Bw. Manampa amesema ni muda mrefu amekuwa akiwaomba
wenyeviti hao kufungua mipaka waliyokuwa wamejiwekea hali ambayo ilipelekea wavuvi haramu
kutumia mipaka hiyo kujificha na kukwepa
doria ya majini.
Katika hatua nyingine Bw. Manampa
ameongeza kuwa kutokana na ushirikiano huo
watapunguza au kuondoa suala la uvuvi haramu ambalo limekuwa na changamoto nyingi
wilayani humo.
Aidha hivi karibuni waziri wa
kilimo ,uvuvi na mifugo dk charlse tizeba alifika wilayani humo na kuzungumza
na wananchi wa eneo hilo ambapo ametoa onyo kali kwa watu wanao jihusisha na
uvuvi haramu ikiwa ni pamoja na kuongeza adhabu kwa mtu atakae bainika
anajihusisha na vitendo hivyo
Baadhi ya wananchi wa nyamirembe na
nyakakarango bw: ganyanka matele na edward magafu wameipongeza
serikali kwa jitihada za kupambana na matumizi ya zana haramu za uvuvi ikiwa ni
njia ya kutokomeza uvuvi haramu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment