Mwenyekiti wa soko la Chato mjini Bw. Daudi Francisco
amewataka wafanya biashara wa samaki wilayani humo kudumisha usafi katika
maeneo yao ya biashara ili kuepuka magonjwa ya milipuko yanayoweza
kujitokeza kutokana na mvua za masika zinazo endelea kunyesha.
Akizungumza na storm habari sokoni hapo mwenyekiti huyo amesema kuwa hali
ya usafi katika eneo lake inapewa kipaumbele
hasa katika kipindi hiki cha mvua za masika ambazo zinaendelea kunyesha.
Aidha amewataka wafanya biashara wa samaki katika
maeneo yanayo zunguka ziwa victoria kufika katika soko hilo kwa lengo la
kujifunza namna ya kufanya usafi na kuepuka magonjwa ya milipuko yanayo
sababishwa na uchafu.
Kwa upande wa baadhi ya wafanya biashara katika soko
hilo Bi. Zuhura Benedicto na Mariam Said wamesema kuwa hali ya biashara eneo
hilo imekuwa hairidhishi kutokana na serikali kuweka utaratibu wa kuuza samaki
wenye ukubwa wa kuanzia sentimita 25 hadi
50 sababu inayo pelekea watu wenye kipato cha chini kushindwa kumudu
gharama za kununua samaki hao.
Sanjari na
hayo wafanya biashara hao wa samaki wameiomba Serikali kupunguza vipimo vya
ukubwa wa samaki kwani kwa
kufanya hivyo itarahisisha biashara hiyo kuwa na mzunguko mkubwa kutokana na samaki hao kununuliwa na
watu wa aina zote .
No comments:
Post a Comment