Mkuu wa wilaya ya Geita mwalimu Hermani Kapufi
amewataka wananchi kuacha kujenga nyumba za makazi
katika vyanzo vya maji na badala
yake kuvilinda na kuvithamini ili visikauke.
Kauli hiyo imetolewa kutokana na kuwepo kwa baadhi
ya watu wilayani Geita ambao wanajenga
nyumba za makazi katika maeneo ya serikali pasipo kufuata sheria hali inayo changia kuwepo
kwa migogoro ya mara kwa mara baina ya
serikali pamoja na wananchi.
Akizungumza na wananchi wa mamlaka ya mji mdogo wa
katoro hivi karibuni mkuu wa wilaya ya geita mwalimu hermani
kapufi amewataka watu walio vamia katika
maeneo ya serikali ikiwa ni pamoja na vyanzo vya maji na kujenga nyumba za
makazi pasipo kufuata sheria na taratibu waondoke mara moja na kuya acha maeneo hayo yakiwa wazi.
Aidha baadhi ya wananchi katika eneo hilo Bw. Salmin godfrey na Mashaka yahaya wameeleza kuwa wamefurahishwa na hatua ya mkuu wa
wilaya ya kuzuia watu kujenga nyumba za
makazi katika vyanzo vya maji pamoja na katika taasisi za kiserikali kama shule
na hospital kwani kwa kufanya hivyo
nikuyafanya maeneo hayo kuwa huru
na salama .
No comments:
Post a Comment