Serikali kupitia Mfuko
wa Maendeleo ya Vijana imetoa mikopo yenye thamani ya Shillingi Billioni 1.5
kwa vikundi vya vijana 129 katika Halmashauri mbalimbali nchini.
Hayo yamebainishwa na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipokuwa
akitoa hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya
mapato na matumizi ya fedha za Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha
2017/2018.
“Serikali inaendelea
na azma yake ya kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kwa kutoa mikopo yenye
riba nafuu”’ Alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Aidha , Mamlaka za
Serikali za Mitaa kupitia mapato yake ya ndani zimetoa Shillingi Billioni 4.6
ikiwa ni mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi vya vijana 2,356 na hatua hizi
zimekwenda sanjari na utengeji wa maeneo maalum yenye jumla ya ekari 85,603 kwa
ajili ya shughuli za vijana za Kilimo, biashara ndogo ndogo, burudani na
michezo.
Katika mwaka
2017/2018, Serikali itaendelea kusimamia Halmashauri zote nchini kutenga
asilmia 5 ya mapato yao kwa ajili ya vijana na asilimia 5 kwa wanawake.
No comments:
Post a Comment