Naibu Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Hamis kigwangalla akijibu
hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la
11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Serikali kupitia
Halmashauri zilizo katika maeneo ya migodi imeanza kuweka mikakati ya kudhibiti
magonjwa ya Kifua kikuu na Silicosiskwa kutoa Elimu kwa
wachimbaji wa madini ikiwemo kujikinga na vumbi na kutumia njia
sahihi za uchimbaji.
Hayo yamesemwa na Naibu Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kingwangalla leo Bungeni Mjini
Dodoma wakati wa Maswali na Majibu.
“Tanzania inafahamu
changamoto ya uwepo wa magonjwa haya ya kifua kikuu na Silicosis
katika maeneo ya wachimbaji, kwa upande wa Kifua kikuu tatizo hili ni kubwa
lakini kuwekuwepo na ripoti za wagonjwa wachache wa Silicosis katika
hospitali za Serikali ikiwemo Kibong’oto”,Alibainisha Mhe.Kigwangalla.
Ameeleza kuwa kupitia
ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Magonjwa ya UKIMWI,Kifua Kikuu, na
Malaria wa Global Fund to Fight AIDS,Tuberculosis na Malaria nchi kumi
wananchama wa jumuiya ya SADC ikiwemo Tanzania ziko katika utekelezaji wa
mpango wa kudhibiti kifua kikuu na magonjwa ya mfumo wa hewa yatokanayo na
uchimbaji madini ikiwemo Silicosis.
Aidha katika mpango
huo kuna afua itakayo shughulika na sera za udhibiti wa
vumbi katika maeneo ya wachimbaji ambayo itawabana wachimbaji kudhibiti vumbi
wakati wa shughuli za uchimbaji.
“Serikali itaongeza
wigo wa huduma katika vituo vya afya kwenye maeneo yaliyoathirika ikiwemo
Mkoa wa Geita ili vituo viwe na uwezo wa kuchunguza na kutibu magonjwa haya na
kuwajengea uwezo wataalamu wa afya katika kuhudumia wagonjwa katika maeneo ya
migodi”Alisisitiza Mhe. Kingwangalla.
No comments:
Post a Comment