Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akitoa tamko kuhusu Siku ya Malaria Duniani kwa waandishi wa
Habari Mjini Dodoma na kusisitiza kuwa vipimo vya Malaria na Dawa za Mseto ni
bure kwa vituo vyote vya Afya vya Umma nchini.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akikata utepe kuzindua Kitabu cha Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria
katika kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani.
Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha
ya pamoja na Wawakilishi kutoka kamouni ya Gullin Pharma mara baada ya kuzindua
Kitabu cha Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria katika kuadhimisha Siku ya Malaria
Duniani.
Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa
Serikali haitosita kuwachukulia hatua mtumishi yoyote katika vituo vya Afya vya
Umma nchini watakaobanika kutoza fedha katika kutoa huduma ya vipimo vya
malaria na kuuza dawa za Mseto kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo.
Ameyasema hayo Mjini
Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari kutoa tamko la Siku ya Malaria
Duniani na kusisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kupata huduma ya kupima malaria
pamoja na dawa za kutibu malaria bure katika vituo vya Afya vya Umma.
“Huduma ya kupima
Malaria na dawa za Mseto zinatakiwa kutolewa bure katika vituo vyote vya Umma
vya Huduma za Afya nchini na hatutosita kuwachukulia hatua watakaokiuka
kutekeleza agizo hili.Alisistiza Mhe. Ummy.
Aidha amwewaagiza
Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kutekeleza agizo hilo na kulisimamia kwa
karibu ili kuondoa usufumbu kwa wananchi wanapotaka kupatiwa huduma hiyo.
Mhe Ummy Mwalimu
amewashukuru wadau wote waliochangia kwa hali na mali katika mafanikio
yaliyofikiwa ya mapambano ya dhidi ya Malaria nchini.
Siku ya Malaria
Duniani uadhimishwa kila Aprili 25 ya kila mwaka na kwa mwaka huu kauli mbiu ni
“ Shiriki kutokomeza Malaria kabisa kwa Manufaa ya Jamii”.
No comments:
Post a Comment