Serikali imesema kuwa
kuanzia mwaka 2013 hadi 2017 vifaranga 67500 vilivyoingizwa nchini kinyume na
sheria viliteketezwa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvivu
Mhe.William Ole Nasha leo Bungeni Mjini Dodoma wakati wa Maswali na Majibu.
“Wako wawekezaji
wachache ambao hupewa vibali maalum vya kuingiza mayai au
vifaranga wa kuku wazazi (Parents Stock) tu,ukaguzi kwa ajili ya kudhibiti
uingizaji vifaranga na mayai unaendelea na hatua kali zinachukuliwa kwa yeyote
anayekamatwa kwa kukiuka utaratibu”,Alisisitiza Mhe.Ole Nasha.
Amesema kuwa kuanzia
mwaka 2006 serikali iliweka katazo la kuingiza kuku na mazao yake nchini ili
kudhibiti ugonjwa hatari wa Mafua ya Ndege na hakuna mwekezaji yeyote
aliyeruhusiwa kupewa kibali cha kuingiza vifaranga au mayai nchini kwa ajiri ya
biashara.
Aidha amesisitiza kuwa
Sheria ya Magonjwa ya Wanyama na .17 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2007
na 2010 zinatumika kudhibiti na kukagua uingizaji katika maeneo ya
mpakani,bandarini na viwanja vya ndege.
No comments:
Post a Comment