Wednesday 5 April 2017

PICHA: MAMA SAMIA SULUHU AWAPA BARAKA SERENGETI BOYS



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na vijana wa timu ya Taifa ya  mpira wa miguu chini ya miaka kumi na Saba “Serengeti Boys”(hawapo pichani) katika hafla ya chakula cha jioni aliyowaandalia vijana hao jana Jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda kuweka kambi ya wiki tatu nchini Morocco ya maandalizi ya kwenda nchini Gabon kushiriki michuano ya kombe la Afrika.Wa kwanza kulia ni Mhe. Rashidi Ally Juma Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Zanzibar na katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akitoa maelezo yanayohusu maandalizi ya timu ya Taifa  ya mpira wa miguu chini ya miaka kumi na Saba “Serengeti Boys” katika hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya kuwaaga wachezaji hao  iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan (kushoto) iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment