Friday 14 April 2017

TATIZO LA UDUMAVU LIPO KWA ASILIMIA 40.5% MKOANI GEITA

Gaudencia Gibay ambaye ni Afisa Lishe wa Shrika lisilo la Kiserikali la IMA WORLD HEALTH akitoa mafunzo kwa maafisa Kilimo na Lishe ambao wanatoka kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Geita.
Afisa Lishe kutoka Taasisi ya Lishe Nchini Bi,Mary Kibona akitoa semina juu ya namna ya kumtunza mama mjamzito na mtoto.
Wanasemina wakisikiliza kwa makini kile ambacho kilikuwa kikielekezwa.
Katibu tawala  wa Mkoa wa Geita ,Selestine Gesimba akifunga mafunzo hayo uku akiwasisitiza wanasemina kutumia vyema kile walichofundishwa.
Gaudencia Gibay ambaye ni Afisa Lishe wa Shrika lisilo la Kiserikali la IMA WORLD HEALTH akitoa maelezo ya chakula cha mfano cha mtoto kwa Katibu tawala  wa Mkoa wa Geita ,Selestine Gesimba 
Joseph Machibya mwenyekiti wa mafunzo hayo akimshukuru Katibu tawala kwa kufika na kufunga mafunzo hayo.
Godfrey Mbaruku ambaye ni Mratibu wa Mawasiliano Mradi wa Mtoto Mwerevu akitoa ufafanuzi juu ya semina ambayo wamewawezesha maafisa kilimo na lishe Mkoani Geita.





Mkoa wa Geita unakabiliwa na tatizo la udumavu kwa kiwango cha asilimia 40.5 ,na hii inatokana na tatizo la baadhi ya kabila kuwa na unyanyapaa kwenye swala la chakula kwa wakina mama wajawazito.

Akifunga mafunzo ya siku tatu  yaliyokuwa yameandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la IMA WORLD HEALTH  kwa maafisa kilimo na watu wanausika na sekta ya afya ambao wanatoka halmashauri tano zilizopo Mkoani Hapa,Katibu tawala  wa Mkoa Huo,Selestine Gesimba amesema kuwa ni vyema kwa watendaji hao wakatumia nafasi hiyo kuakikisha wanapambana na tatizo la udumavu na kutoka kwenye asilimia iliyopo kwa sasa.
“Natoa maelekezo kwamba kama wewe umeshiriki kikamilifu katika mafunzo haya basi ni matarajio yangu kuwa nitaona mabadiliko makubwa katika jamii,na hivyo suala la UDUMAVU litapungua kwa kiasi kikubwa Mkoani kwetu”Alisisitiza Gesimba.

 Afisa Lishe kutoka taasisi ya chakula Lishe nchini Bi,Mary Kibona ambapo ameelezea kuwa hali ya udumavu nchini hapa ni kubwa kwani ni asilimia 34.5 ya watoto wanashida  hiyo.
“Hali ya UDUMAVU sio nzuri nchini kwetu hususani katika Mikoa ambayo inalima chakula kwa wingi kwa Mfano,Kagera ,Mara na Geita ni miongoni mwa mikoa ambapo tatizo hili ni kubwa sana”Alisema Bi,Kibona.

Baadhi ya washiriki kwenye semina hiyo  Bi Magdarena Thomas na Joseph Machibya wameelezea kuwa jamii ambayo hipo Mkoani Hapa bado ni tatizo kwani wengi bado awajatambua swala la rishe kwa mtoto na mama mjamzito.


Kutokana na hali ilivyo ya Tatizo Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kushirikiana na Serikali ya Uingereza kupitia shirikia la IMA world Health chain ya mradi wa Mtoto Mwerevu,limeonelea kuanzisha mpango huu kwaajili ya kupambana na Tatizo la UDUMAVU.

No comments:

Post a Comment