Naibu Waziri wa Kilimo
Uvuvi na Ufugaji Mhe. William Ole Nasha akijibu hoja mbalimbali za wabunge
katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mjini Dodoma.
Serikali imesema kuwa
inaandaa utaratibu wa kuunda Bodi mpya ya wakurugenzi ya Tumbaku kwa
kuwa ina umuhimu mkubwa katika ukuaji wa Sekta ya Tumbaku nchini.
Hayo yamebainishwa na
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha wakati
akijibu hoja mbalimbali za wabunge mjini Dodoma.
“Serikali ilivunja
Bodi ya Tumbaku kwa lengo la kufanya maboresho katika utendaji kazi wa Bodi,na
hatua hii ya kuvunja Bodi ya wakurugenzi haihusu kusitisha shughuli
zinazotekelezwa katika sekta hii ya tumbaku kwani wapo wataalamu wanaoendeleza
utekelezaji wa mpango uliopo wa kuendeleza zao la tumbaku”. Aliongeza Mhe.Ole
Nasha.
Aidha amesisitiza kuwa
upatikanaji wa pembejeo za zao hilo zitapatikana kupitia vyama vikuu vya
ushirika kwa kila eneo kwa kupitia mchakato wa zabuni unaosimamiwa na
kuratibiwa na vyama vikuu vya ushirika.
Amezitaja pembejeo za
muhimu kwenye zao la tumbaku kuwa ni mbolea aina ya NPK, Mbolea aina ya CAN,
nyuzi za kufungia tumbaku wakati wa kuvuna na wakati wa masoko zote
zitapatikana kupitia vyama vikuu vya ushirika.
Ameeleza kuwa kwa
kuzingatia kuwa wakulima wanahitaji huduma muhimu hasa katika
kipindi hiki cha kuelekea masoko ya tumbaku kwa msimu wa 2017/18, Serikali
imeateua timu kwa ajili ya uratibu na kusimamia masuala hayo.
“Tuna timu tayari iko
mkoani Tabora ambayo itasimamia na kuratibu masuala mbalimbali ya wakulima
ikiwa ni pamoja na kuandaa upatikanaji wa pembejeo kwa msimu ujao,hivyo pamoja
na WETCU kuvunjwa kazi za chama hicho zinaendelea kama kawaida”Alisema Mhe.Ole
Nasha.
No comments:
Post a Comment