Naibu katibu Mkuu akimpongeza moja kati ya wananchi ambaye ameamua kujiunga na CCM.
Naibu katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Bara Rodrick Mpogolo amekutana na wajumbe wa sekretalieti za chama Wilaya zote zilizopo Mkoani
Geita na kuwasisitiza wananchama hao
kuwa na umoja na upendo ndani ya chama huku wakiwa na umoja kwenye shughuli
ambazo zinausiana na chama hicho.
Mpogolo amesisitiza hayo wakati wa kikao cha maelekezo
kilichofanyika kwenye ukumbi wa
halmshauri ya mji wa Geita mjini humo,alisisitiza kuwa ni wakati wa wananchama
kuakikisha wanajenga umoja hili chama hicho kuwa imara na chenye nguvu ambacho
kitaendelea kuchukua .
“Lazima kwanza wanaccm tubadirike tuanze kuwa na umoja ndani
ya chama chetu tuachane na unafiki,majungu chuki na fitina maana hata imani ya
chama chetu kinaamini kuwa swala la umoja na usawa ni msingi ambao upo ndani ya
chama chetu”Mpogolo aliwasisitiza wanachama.
Aliongeza kuwa endepo kama wanachama wataeshimiana na
kupendana hakika chama kitaendelea kuleta
mageuzi makubwa ndani ya chama na kwamba kazi iliyopo ni kuongeza wanachama
ndani ya CCM na kwamba lazima kila
mwanachama awe na uwezo wa kushauri kwa watu kujiunga na chama hicho.
Aidha kwa Upande Mwingine amehimiza swala la maadili na
kupinga vikali maswala ambayo yanaweza kukichafua chama hicho kama mambo ya
Rushwa na kutokutambua haki za kila
mwanachama ambaye yumo ndani ya chama hicho.
Katibu pia amewataka viongozi wa chama kusimamia ilani ya
uchaguzi katika maeneo yao kwa weledi mkubwa ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoani
Humo Joseph Kasheku Msukuma amemwakikishia
Naibu Katibu Mkuu kuyafanyia kazi maelekezo ambayo ameyatoa huku
akiwasisitiza viongozi kuzingatia misingi ya haki na usawa kwa kuwatumiakia
wananchini na kwamba yale ambayo yamesemwa inawezekana endepo kwa kila kiongozi
na mwanachama hakitimiza wajibu wake.
|
No comments:
Post a Comment