Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge akijibu hoja
mbalimbali za wabunge katika akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao
cha pili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Serikali kwa
kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, Benki ya
Maendeleo ya Waarabu(BADEA),Washirka wa Maendeleo (DPS), na Serikali ya India kwa
pamoja wametoa jumla ya Shillingi Billion 164 kawa ajili ya kutekeleza mradi wa
maji Chalinze kwa awamu tatu.
Akijibu Swali Mbunge
wa Chalinze (CCM) Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete lililouliza kuwa Wakazi wa
Chalinze wamekuwa katika sintofahamu ya kukamilka kwa mradi wa maji Chalinze?
Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge ameeleza kuwa Serikali ipo katika
utekelezaji wa mradi huo na gharama za utekelzaji wake ni Shillingi Billioni
23.4 kwa awamu ya kwanza na Shillingi Billioni 53.7 kwa awamu ya pili ya mradi
na kwa awamu ya tatu itagharimu Shillingi Billioni 86.9.
Ameongeza kuwa
kukamilika kwa awamu ya kwanza na utekelezaji umekamilika na kwa awamu ya pili
ya mradi huo jumla ya vijiji 88 vimenufaika na kupeleka hali ya upatikanaji wa
maji katika mji wa Chalinze na Vitongoji vyake kufikia asilimi 88 ya wakazi
wote waishio katika eneo lote linalopitiwa na mtandao wa maji.
“Mradi upo katika
hatua nzuri na umekamilika kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili ipo katika
utekelzeaji na wanachi wameanza kunufaika na mradi huu kwa kupata huduma ya
maji” alisisitiza Mhe. Lwenge.
Pia ameleza kuwa
katika awamu ya pili vijiji 12 vya Mwindu,Visakazi, Lulenge,
tukamisasa,Kinonko, Bwawani, Sinyaulime, Gwata, Ngerengere, Kidugalo, Kambi ya
Kinonko na Sangasanga vitaanza kupata huduma ya maji ifikapo mwishoni mwa mwezi
Aprili mwaka 2017 baada ya kukamilika kwa majaribio ya bomba kuu.
Vijiji vitatu vya
Kwang’andu,kifuleta na Kwaruhombo vitaanza kupata maji mara baada ya mkandarasi
kufanya maboresho ya pampu ambazo zimeonekana hazifanyi kazi kama inavyotakiwa na
mkandarasi huyo ameagizwa kuhakikisha pampu hizo zinafanya kazi
kabla ya Juni 2017.
Aidha
kwa sasa Serikali inatekeleza mradi huu kwa awamu ya tatu ambapo upanuzi wa
mtambo wa kuzalisha maji, ujenzi wa mabomba makuu ya kusafirisha maji (KM 115),
Ujenzi wa mfumo wa manomba ya kusambaza maji(KM 1022), Ujenzi wa matanki
makubwa 19 na ujenzi wa vituo 9 vya kuchotea maji na ujenzi wa vioski 351 vya
kuchotea maji vinatekelzwa.
No comments:
Post a Comment