Watu watatu wakazi wa mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani na
mkoani Geita wamekamatwa baada ya kukutwa katika msitu ambao umezuiwa kufanyika
shughuli za kibinadamu huku wakiwa wanakata
miti.
Wakizungumza watu hao ambao wametambulika kwa majina
ya Paskali Songano , John Zakaria na Lukas Philipo wote wakazi wa mtaa wa mtoni katika mamlaka ya mji mdogo
wa katoro ambapo wamesema kuwa waliingia
katika msitu huo kwa lengo la kukusanya magogo kwa ajili ya kuyatumia katika
shughuli za uchomaji wa
matofari .
Sanjari na hayo watu hao wamesema kuwa kabla ya
kuingia katika msitu huo walipita kwa mwenyekiti wa eneo hilo na
aliwaruhusu kuingia katika msitu
huo kuchukua magogo ya visiki vya miti
kwa kuchangia kiasi cha pesa
taslimu shilingi elfu ishirini na kiongozi huyo aliwapatia stakabadhi ya halmashauli ya wilaya ya geita
kama kielelezo pindi wapatapo matatizo
msituni humo.
Kwa upande wake mlinzi wa msitu huo alie husika kuwakamata watu hao Bw.Zabroni Peter
ameeleza kuwa amewakuta watu hao wakiwa
wanakata miti kwakutumia shoka walizo
kuwa nazo na siyo kwamba walikuwa
wanakusanya magogo kama wanavyo eleza wao.
Aidha mwenyekiti wa mtaa huo Bw. Masunga Mbishi
amekiri kuwapatia kibali cha kuwaruhusu watu hao kuingia katika msitu huo kwa
lengo la kuchukua magogo na siyo kukata miti kama inavyo elezwa .
Bw. Masunga
amesema watu hao waliokamatwa na mlinzi
wa msitu huo hawana hatia kwasababu yeye ndiyo aliyewapatia ruhusa ya kuingia
katika eneo hilo kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya miti ambayo imeharibiwa
vibaya na watu wasio julikana.
Mpaka sasa watu hao wameachiwa huru.
No comments:
Post a Comment