Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula
Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa shule ya Msingi Kalangalala Mkoani Geita.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba alipotembelea banda la Kampuni ya POLYTECH MACHINERY inayojishughulisha na uuzaji wa mashine mbalimbali ikiwemo za kukamua mafuta ya alizeti wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula
Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita. Mwingine ni Mhe Dkt Mary Mwanjelwa Naibu waziri wa Kilimo (Kulia).
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita ,Celestine Gesimba akiwatambulisha baadhi ya wageni wa Kitaifa na Mkoa wakati wa maadhimisho ya siku ya chakula Duniani. |
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa maadhimisho ya siku ya chakula wakiendelea kufuatilia. |
Mwigizaji maarufu wa kikundi cha Futuhi Brother K akionesha makeke yake kwenye maadhimisho ya Wiki ya chakula. |
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akitoa salaamu za Wizara ya Kilimo na kuelezea Chimbuko la Siku ya chakula Duniani ambayo ilianzishwa mwaka 1979 . |
Diwani wa Kata ya Buseresere Godfrey Miti akipatiwa cheti na Waziri wa Kilimo Charles Tizeba cha ushiriki kwenye maadhimisho hayo. |
Mbunge wa Jimbo la Busanda ,Lolesia Bukwimba akiwashukuru wananchi ambao wamejitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya chakula. |
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula
Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Na JOEL MADUKA
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba leo
Octoba 16, 2017 amefunga rasmi maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula
Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita kuanzia
Octoba 10 mpaka Octoba 16, mwaka 2017.
Akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho hayo waziri Tizeba alisema
kuwa Uzalishaji wa
mazao ya chakula kwa mwaka 2016/2017 umefikia tani 15,900,864 za chakula kwa mlinganisho wa nafaka. Kati ya kiasi
hicho, tani 9,388,772 ni za mazao ya
nafaka na tani 6,512,092 ni za mazao
yasiyo nafaka. Mahitaji ya chakula kwa
mwaka 2017/2018 yatakuwa tani 13,300,034
ambapo tani 8,457,558 ni kwa mazao
ya nafaka na tani 4,842,476 ni mazao
yasiyo nafaka.
DktTizeba alisema kutokana na uzalishaji huu, nchi itakuwa na kiwango cha utoshelevu wa asilimia 120 ambapo kiwango hiki kinaonyesha kuwa nchi itakuwa na ziada ya chakula ya tani 2,600,831 ambapo mazao ya nafaka kutakuwa na ziada ya tani 931,214 na mazao yasiyo nafaka ni tani 1,669,617 kwa viwango vya utoshelevu vya asilimia 111 na 134 mtawalia.
DktTizeba alisema kutokana na uzalishaji huu, nchi itakuwa na kiwango cha utoshelevu wa asilimia 120 ambapo kiwango hiki kinaonyesha kuwa nchi itakuwa na ziada ya chakula ya tani 2,600,831 ambapo mazao ya nafaka kutakuwa na ziada ya tani 931,214 na mazao yasiyo nafaka ni tani 1,669,617 kwa viwango vya utoshelevu vya asilimia 111 na 134 mtawalia.
Dkt Tizeba aliendelea kusema Madhumuni ya Maadhimisho
ya Siku ya Chakula Duniani ni kutoa nafasi ya kutafakari, namna Jamii katika
ngazi ya Kaya, Kijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa, Taifa na Kimataifa zinavyoweza kuhakikisha ongezeko la
uzalishaji na upatikanaji wa chakula cha kutosha na chenye lishe bora kwa watu
wote na kwa wakati wote.
Kaulimbiu ya mwaka huu 2017 inasema “Badili mwelekeo wa uhamaji; Wekeza katika
usalama wa chakula na maendeleo Vijijini”. Kaulimbiu hii inaweka umuhimu katika kuweka Mipango na
Programu zinazolenga kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo
Vijijini; kupuza utegemezi na kuongeza usawa katika Jamii, sambamba na uhifadhi
mazingira ambayo ndiyo muhimu katika maendeleo ya kilimo na hifadhi ya Jamii
ili yachochee jitihada za kuondoa umaskini.
Alisema kuwa maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani
kwa mwaka huu ni ya kujivunia kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana
katika uongozi wa Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli, kwa kipindi
chote nchi yetu imejitosheleza kwa chakula kwa zaidi ya asilimia 100 na hivyo
kuwa na ziada ya chakula.
Katika hatua nyingine Mhe waziri wa kilimo ametumia fursa hiyo kuwaasa wananchi wote kuwa na hifadhi ya chakula katika kaya zao na kutumia chakula kilichopo kwa uangalifu hadi msimu mwingine wa mavuno.
No comments:
Post a Comment