Mkuu wa
wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akitoa maagizo wakati wa mkutano wa kusoma
mapato na matumizi uliofanyika kwenye kijiji cha Lwamgasa.
Mtendaji wa
kijiji cha Lwamgasa ,Samwel Shosha akisamo taarifa ya mapato na matumizi ya
kijiji.
Mkuu wa
wilaya pamoja na Diwani wa Kata ya Lwamgasa wakifatilia kwa makini taarifa ya
mapato na matumizi ya kijiji
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya
ya Geita Mwl.Herman Kapufi kwenye mkutano mkuu wa kijiji hicho baada ya
wataalam wa hesabu za ndani katika Halmashauri ya wilaya kutokubaliana na
taarifa ya mtendaji wa kijiji hicho Bw. Samuel Shosha.
“Mwenyekiti wa serikali ya kijiji,
mtendaji na serikali yote ambao walikuwa wamepitisha mihtasali yote, Mkaguzi wa
ndani, kamati ya ulinzi na usalama tukutane ofisini kwangu tarehe mbili mwezi
wa pili muda wa saa tatu kamili lakini mwenyekiti wa kijiji unapokuja uje na
mihtasali yote,stakbadhi na nyaraka zote sitaki tena kisingizio lakini pia
mnatakiwa mje na daftari ambalo linaorodha ya mali zote zinazomilikiwa na
serikali”Alisisitiza Kapufi
Katika mkutano huo,Afisa mkaguzi wa
ndani Chacha Marwa amesema fedha zote za serikali zinatakiwa kuwa na vielelezo
pamoja na nyaraka zinazoainisha matumizi jambo ambalo halikuzingatiwa
Akifunga mkutano huo,mwenyekiti wa
kijiji Bw.Lumumba Salvatory amekanusha matumizi mabaya ya fedha hizo,huku
akisema kuwa hali hiyo inachochewa na Itikad za kisiasa ili kukwamisha jitihada
za serikali ya kijiji hicho.
No comments:
Post a Comment