Wasambazaji wa Filamu
na Muziki nchini wameashauriwa kuzingatia na kufuata Sheria za nchi katika
usambazaji wa kazi hizo.
Ushauri huo umetolewa
leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na
Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokutana na Umoja wa Wasambazaji wa Filamu na
Muziki kujadili mustakabali wa usambazaji wa kazi za Sanaa nchini.
“ Nia yangu njema
sina nia ya kumuumiza mtu nataka sheria na taratibu zilizopo
zifuatwe mnapotekeleza majukumu yenu ya usambazaji wa Filamu na muziki” alisema
Mhe. Nape.
Mhe. Nape Moses Nnauye
amewahakikishia wasambazaji hao kuwa Serikali ipo pamoja nao na watashirikiana
kwa pamoja ili kuweza kutafuta namna bora ya kuboresha usambazaji wa Filamu na
Muziki nchini.
Mhe. Nape ameongeza
kuwa yuko tayari kupokea mawazo na ushauri kutoka kwa Wasambazaji wa Filamu na
Muziki nchini katika kupata namna nzuri ya kutatua changamoto zilizopo na
kuboresha njia za usambazaji wa kazi za Sanaa.
Naye Mwakilishi wa
Umoja wa Wasambazaji wa Filamu na Muziki nchini Bw. Joseph Lyakurwa
amempongeza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
kwa jitihada za Serikali katika kupambana na wizi wa kazi za Sanaa nchini na
kuomba kuendelea na kuwasaka na kuwachukulia hatua wote wanaokiuka Sheria na
taratibu katika usambazaji wa kazi za Sanaa.
“ Nakuomba Mhe. Waziri
tukishalipa kodi zote zinazotakiwa kwa mujibu wa Sheria na taratibu zilizopo
baada ya hapo mfanyabiashara atakayekamatwa amekiuka Sheria na taratibu hatua
kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake”.alisema Bw. Lyakurwa.
Kwa upande wake Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amewashauri
Wasambazaji wa Filamu na Muziki kuzingatia ubora wa kazi wanazozisambaza ili
kuweza kushindana na soko la filamu na muziki wa nje.
“ Nawaomba wasambazaji wa Filamu na
Muziki muzingatie ubora wa kazi mnazo zisambaza kwani tunashindana na filamu za
jje kwahiyo tukizingatia hilo Filamu na Muziki wetu utasonga mbele”
Alisema Bibi. Joyce.
Baada ya kikao hicho
baina ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na
Umoja wa Wasambazaji wa Filamu na Muziki nchini,kamati ya watu saba imeundwa
kukaa na kujadiliana na kupata suluhisho la namna bora ya usambazaji wa kazi za
Sanaa na kuwasilisha ripoti kwa Mhe. Waziri.
No comments:
Post a Comment