Friday 19 August 2016

WAENDESHA PIKIPIKI(BODABODA) WILAYANI MBOGWE MKOANI HAPA WALALAMIKIA JESHI LA POLISI


Waendesha  Pipikipi maarufu kwa jina la bodaboda wa Masumbwe Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wamelalamikia jeshi la Polisi  wilayani humo kutokana na baadhi ya askari  wa jeshi hilo kukamata pikipiki zao mara kwa mara na kuwaacha na hali ya umasikini inayosababisha kukoswa fedha za kuhudumia familia zao
Wakizungumzia hili baadhi ya waendesha bodaboda Joseph Msani na Mtulivu Shabani  wamesema mara nyingine wanakuwa wametimiza vifaa na vielelezo vyote vinavyohitajika kwa ajili ya vyombo vyao ikiwemo kuvaa kofia ngumu (element), lakini bado polisi wamekuwa wakiwakamatana hivyo kuonekana kama ni vitega uchumi kwa Askari hao na pindi wanapowakamata wanakuwa wamevalia nguo za nyumbani hali ambayo imekuwa  ikiwapa  wasiwasi.

Kero hii ya bodaboda pamoja na kwamba ipo kwa muda sasa lakini imeonekana kuwagusa Wajumbe wa Jumuiya ya wazazi wa CCM wilaya ya Mbogwe

Aidha Mwenyekiti wa Jumuiya ya  Wazazi CCM Mkoa wa Geita, Dotto Biteko mara baada ya kupokea changamoto hizo  amehaidi kuhakikisha anazungumza na RPC kujua tatizo hilo ambalo limekuwa ni kero kwa waendesha  boda boda.


Nae mwenyekiti wa ulinzi na usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya mbogwe Matha Mkupasi  ambapo amesema kuwa jitihada zilizokuwepo kwa sasa ni kuhakikisha wanawapatia elimu ya kutosha waendesha bodaboda ili kuepukana na matatizo na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani.

No comments:

Post a Comment