Diwani wa Kata ya Nyankumbu akiendesha zoezi la kutoza ushuru kwa baadhi ya wafanyabiashara
Baadhi ya wanunuzi wa Bidhaa katika Soko hilo
Wafanyabiashara
wadogo wa mboga mboga na matunda katika Soko la Nyakumbu lililopo Kata
ya Nyakumbu Wilayani na Mkoani Geita,wamelalamikia kitendo cha Diwani wa Kata
hiyo Bw.Michael Kapaya kuwatoza Ushuru
wa Sh.200 kwani hivi karibuni kumekuwepo
na agizo kutoka kwa Rais John Magufuli la kutokuwabughuzi wafanyabiashara
wadogo.
Wakizungumzia sakata hilo baadhi ya wafanyabiashara Bi.Thabiza
Shuli ,Suzana Enock na Bw. Julius Charles ambao wanafanya biashara katika soko
hilo wamesema kuhusiana na kuchangia
gharama za usafi wa soko wamekuwa wakilipa lakini hawaoni usafi unaofanyika
hali ambayo imewasababisha kuwa wagumu wa kutoa ushuru huo na sababu nyingine
wakieleza ni diwani kuingilia majukumu ambayo si ya kwake kwani majukumu hayo
ni ya mtendaji wa Kata au Mtaa husika.
Katibu wa Soko hilo Bw.Philimon Charles,ameelezea
kuwa kutokana na suala hilo yeye kama kiongozi anajua kuwa nafasi ya Diwani ni kuhakikisha
anahimiza watu kutoa ushuru lakini yeye sio kusimamia zoezi la kuwatoza ushuru
wafanya biashara hao.
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Michael Kapaya ameeleza kuwa kufikia uamuzi huo ameshakutana
na Mtendaji na Viongozi wengine na mwisho wa siku aliamua kufanya hivyo kwa
lengo la kutoza fedha hizo ili usafi ufanyike katika soko hilo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji mhandisi Modesti Hapolinali
amesema kuwa Diwani jukumu lake kubwa ni
kuwahimiza wafanyabiashara kutoa ushuru na sio kutoza fedha na kwamba katika
soko hilo kuna watu wamekwisha wekwa kwa
ajili ya kutoza fedha na wanahusika ni wale ambao wana meza za biashara ndani
ya soko hilo ndio wanahusika kutozwa fedha lakini sio wale ambao wapo nje ya
soko
No comments:
Post a Comment