Tuesday 2 August 2016

MANJI AITISHA MKUTANO WA DHARULA YANGA BAADA YA DEWJI KUKUBALIWA KUINUNUA SIMBA

MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Manji ameitisha Mkutano wa dharula wa wanachama utakaofanyika Jumapili wiki hii Bwalo la Maofisa wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
Manji anaitisha Mkutano huo siku mbili tu baada ya wapinzani, Simba SC kuamua kuingia katika mfumo wa kuuza hisa kufuatia Mkutano wao wa Jumapili hapo hapo, Bwalo la Maofisa wa Polisi.

Barua ya tangazo la Mkutano wa Yanga haijataja agenda – na Mkutano huo unakuja miezi miwili tu mno tangu kufanyika kwa uchaguzi Mkuu Juni 11, mwaka huu.

Simba imekubali mabadiliko kutoka klabu kuwa mali ya wanachama wote na kuamua kuuza hisa – na tayari bilionea Mohamed Dewji ametoa ofa ya kununua asilimia 51 ya hisa za klabu kwa Sh. Bilioni 20.

Wakati huo huo: Yanga SC itakuwa na mchezo wa kirafiki Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, yakiwa ni maandaliai ya mchezo wao wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika wiki ijayo dhidi ya MO Bejaia ya Algeria.

No comments:

Post a Comment