Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
akizungumza na wadau wa Michezoalipokuwa akizindua uzinduzi wa Channeli mpya za Michezo kutoka
kampuni ya TING Agosti 28,2016.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya TING Dkt .Veron Fernandez
akielezea kuhusu faida za channeli mbili mpya
za michezo kutoka katika kampuni yake zitakavyosaidia kukuza Michezo
nchini Agosti 28,2016.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akijadiliana
jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
ya TING Dkt. Veron Fernandez wakati wa uzinduzi wa Channeli mbili za Michezo kutoka
Kampuni ya TING Agosti 28,2016.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikata
utepe kuashiria uzindua wa Channeli mbili za michezo ambazo ni TING Michezo HD 1 na TING Michezo HD 2 kutoka
Kampuni ya TING Agosti 28,2016.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Said Kiganja akionesha zawadi ya King’amuzi aliyopewa na Kampuni ya TING wakati wa uzinduzi wa Channeli mbili za Michezo kutoka Kampuni hiyo Agosti 28,2016.
Wadau wa Michezo
nchini wameshauriwa kujenga viwanda kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya michezo
ili kuleta maendeleo katika sekta hiyo.
Ushauri huo
umetolewa jana na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
Wambura alipokuwa akizindua channeli
mbili za Michezo za Kampuni ya king’amuzi
cha TING.
Naibu Waziri
Anastazia alisema kuwa kwa kupitia
uwekezaji huo kutasaidia kuinua sekta ya michezo nchini pamoja na kuondokana na
changa moto ya vifaa vya michezo jezi za michezo,mipira na vifaa vinginevyo.
“Tuunge mkono
juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kuwekeza katika viwanda
vitakavyotengeneza vifaa vya michezo” alisema Mhe. Anastazia
Aidha, Naibu
Waziri huyo aliongeza kuwa kuwepo kwa viwanda hivyo kutasaidia kupunguza tatizo
la ukosefu wa vifaa vya michezo nchini kwani vifaa vingi vya vinatoka nje ya
Tanzania hivyo huuzwa kwa bei ya juu.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TING
Dkt. Veron Frenandes ameishukuru Serikali kwa kutoa ushirikiano kwa wadau mbalimbali wa Michezo nchini katika
kukuza na kuendeleza sekta hiyo.
Chaneli za
Michezo zilizozinduliwa katika Kingamuzi hicho ni ni TING Michezo HD 1 na TING Michezo HD 2 ambazo
zitakuwa zikionesha michezo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.
No comments:
Post a Comment