Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (Kushoto) akijadiliana jambo na Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing(kulia) kabla ya kuanza kwa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (katika) akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing(kulia) kabla ya kuanza kwa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Bw.Lv Youqing.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye akiwasilisha hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam ulikuwa ukijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Bara la Afrika na China.
Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing akiwasilisha hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam ulikuwa ukijadali masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Bara la Afrika na China.
Mshauri wa mambo ya Mawasiliano kutoka Tume ya Umoja wa Afrika Bibi. Doreen Apollos akisema hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umejikita katika kujadili uhusiano wa Afrika na China kupitia Nyanja mbamilmbali ikiwemo mawasiliano na afya.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing(kulia) wakati wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umejikita katika kujadili uhusiano wa Afrika na China kupitia Nyanja mbamilmbali ikiwemo mawasiliano na afya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (wa kwanza kulia) na Balozi wa China nchini Bw. Lv Youqing(wa pili kulia) wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye(hayupo katika picha) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (kushoto) na Balozi wa China nchini Bw. Lv Youqing(kulia) wakionyesha hundi ya shilingi milioni arobaini na tano zilizotolewa na watu wa China kwa ajili ya kuchangia madawati katika shule za msingi za Dar es Salaam.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (katikati waliokaa ) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wakifuatilia
hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wageni waalikwa wakati wa mkutano wa
China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari
,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye amewataka waandishi wa
habari kuwa wazalendo kwa kuandika
habari za maendeleo ya bara la Afrika.
Hayo ameyasema leo
jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public
Diplomacy Forum na kueleza kuwa uhusiano baina ya Afrika na China ni wa muda
mrefu na umejikita katika kuboresha teknolojia ya mawasiliano na hivyo kukuza
uchumi wake.
Aidha aliongeza kuwa ili
bara la Afrika liweze kuelezea historia yake kwa mataifa mingine katika kujiletea maendeleo kuna haja ya kuvijengea uwezo vyombo vya
habari katika kutoa habari nzuri zenye manufaa kwa jamii husika.
“Katika karne hii tuliyopo
sasa kuna mabadiliko mengi ya teknolojia
hivyo ni budi kuendelea
kuimarisha ushirikiano ulipo baina ya China na Afrika ili kuleta maendeleo chanya kwa jamii zetu
kupitia vyombo vya habari huku tukitunza
na kueneza tamaduni zetu” alisema Mhe.Nape.
Waziri Nape alizidi
kufafanua kuwa vyombo vya habari katika nchi za bara la Afrika vina uwezo mkubwa wa kukuza na kueneza utamaduni, kuhudumia jamii,kujenga umoja wa kitaifa na kulinda maslahi ya jamii duniani.
Naye Rais wa China
Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing amesema kuwa anafurahishwa na uhusiano uonaozidi kuimarika baina ya nchi za Afrika na
China na kuahidi kuboresha mawasiliano na mahusiano ili kufikia mafanikio
makubwa yaliyokusudiwa.
Mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum umejikita
katika kujadili mambo mbalimbali ikiwemo mahusiano baina ya mtu na mtu na
Vyombo vya habari,afya,na tiba asilia.
No comments:
Post a Comment