Watu wawili wameuawa kwa kuchomwa moto na watu wasiojulikana kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wavuvi haramu waliokuwa wakifanya shughuli za uvuvi kwa kutumia sumu katika ziwa Victoria na kisha watu hao kubomoa nyumba za mrehemu hao hali ambayo imewalazimu askari kutumia silaha kali ili kuwatawanya watu hao.
Tukio hilo limetokea
majira ya saa kumi usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Nyamalele Kata ya
Nkome mkoani Geita ambapo marehemu mmoja aliyefahamika kwa jina la Franco
Mganda mkazi wa kijiji cha Nkome na mwingine
ambaye bado jina lake halijajulikana wameuwawa na wananchi kisha kuteketezwa
kwa moto.
Wakizungumza baadhi ya
mashuhuda waliofika kushuhudia tukio hilo Bw.Thobias Kapuli na Bw.Tom Samsoni
wamesema kuwa marehemu aliyefahamika kwa jina la Franco alikuwa ni mwendesha
pikipiki ambaye alikuwa ameenda kubeba samaki wanaodaiwa kuwa walikuwa wamevuliwa
kwa njia haramu ndipo akiwa njiani alikutana na watu wasiojulikana wakaanza
kuwashambulia na hatimae kupoteza maisha.
Hata hivyo mkuu wa
Wilaya ya Geita Mwl.Herman Kapufi amefika katika eneo la tukio na kulaani
kitendo hicho huku akiwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria
mkononi na badala yake kutoa taarifa katika vyombo husika ili vyombo hivyo viweze kushughulikia.
Aidha Kapufi
amevitaka vyombo vyote vinavyohusika na
kutoa haki kwa jamii ikiwemo Polisi na Mahakama kutenda haki kwa wananchi ili kuondoa
hasira kwa wananchi pindi wanapokuwa hawajatendewa haki.
Katika hatua nyingine Kamanda wa Polisi Mkoani hapa
Mponjoli Mwabulambo amethibitisha
kutokea kwa tukio
hilo.
No comments:
Post a Comment