Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia)
akimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro
(aliyeinua mkono) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa kikao kazi na baadhi ya watumishi
wa Ofisi ya Rais- Utumishi kuhusu utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA katika
Utumishi wa Umma kilichofanyika katika
ukumbi wa utumishi leo, wa tatu kulia (mstari wa mbele) ni Naibu Katibu Mkuu
Utumishi na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi.
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akielekeza jambo kwa
baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais Utumishi wakati wa kikao kazi kuhusu
utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi
leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na baadhi ya
Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakijadili kuhusu matumizi ya TEHAMA katika
utoaji huduma Serikalini wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa
utumishi leo.
No comments:
Post a Comment