Friday 26 August 2016

MIGOGORO YA FAMILIA YASABABISHA KIFO CHA MTU MMOJA MKOANI GEITA



Mtu  mmoja amejinyonga kwa kamba ya manila na kupoteza maisha kwa kile kinachosadikika kuwa ni migogoro  wa  kifamilia kati ya mke na mume.
Tukio hilo limetokea katika mtaa  wa Bomani  Kata  ya Kantente  Wilayani Bukombe mkoani  Geita.
Mtendaji  wa mtaa huo Annastazia  Atnas amethibitisha  kutokea  kwa tukio hilo,na aliyefikwa na mauti  ni  Gidioni Chiza Balangwiza na  alipo ulizia  chanzo aliambiwa kuwa ni mgogoro ndani  ya nyumba na kwamba mama mwenye mji huo  ametoroka baada  ya kusikia tukio hilo.

Aidha Balozi wa nyumba kumi Deus  Kachine  amesema kuwa  mwanamke ameshawai kupeleka taarifa ya ugomvi wa yeye na mumewe  na kwamba walitakiwa kwenda asubuhi iliyofuatia kwa lengo la kwenda kusuluhishwa ugomvi waliokuwa  nao.

Diwani  wa Kata ya Kantente, Bahati  Kayagira ametoa  rai  kwa  wanajamii kuachana na tabia ya kujichukulia hatua mkononi na pia amewasihii wanawake kuacha kuwa na jaziba na kupenda kusikiliza maelezo kutoka kwa wanaume zao.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani  hapa, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwaasa wananchi kunapotokea  migogoro kufika katika vyombo  vya dola  kuliko   kuendelea kujichukulia   mamlaka mkononi.


No comments:

Post a Comment