Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani
Geita la kuwagawia wananchi mabaki ya mawe maarufu kama Magwangala kutoka mgodi
wa dhahabu wa Geita GGM umeanza kutekelezwa.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo yupo
katika ziara ya kikazi katika mgodi huo kwa kutafuta sehemu ambayo wachimbaji
watayaweka na kuyachenjua kwa ajili ya kuyagawa kwa wananchi.
Akiongea mara baada ya ziara hiyo Mhe. Muhongo amesema
kuwa agizo la Rais lilikuwa ni baada ya wiki tatu lakini kwa kuwajali wananchi
wa eneo hilo wameamua kuanza zoezi hilo mapema kwa ajili ya utekelezaji wa
agizo la rais.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali
Emanuel Kiunga, amesema kuwa serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na wabunge wa
mkoa huo na baadhi ya viongozi wametafuta maeneo ya kuweka Magwangala hayo kwa
ajili ya kuyahifadhi.
Wakizungumzia maeneo hayo yaliyotengwa kwa ajili ya zoezi
hilo baadhi ya wabunge wa mkoa huo akiwemo Mbunge wa viti Maalum kwa tiketi ya
CHADEMA, Upendo Peneza, na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Musukuma
wamesema serikali lazima iwe makini na mawe hayo pamoja na kuwajali wananchi wa
maeneo yaliyotengwa.
No comments:
Post a Comment