Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula
Mashauri(katikati aliyesimama) akizungumza na mafundi wa TEMESA wakati akifunga
mafunzo ya mafundi wa Wakala hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Kaimu Mtendaji TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan(kulia) akitoa neno kwa
mafundi wa TEMESA wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao
iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016
kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula
Mashauri .
Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula
Mashauri akionesha moja ya vifaa vilivyokabidhiwa na mafundi wa TEMESA kwa
ajili ya karakana zao wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao
iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula
Mashauri akikabidhi cheti kwa mmoja wa mafundi Bw.Saidi Waziri kutoka Arusha
wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo
cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula
Mashauri akikabidhi moja ya vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya karakana za TEMESA
kwa Bw. Japhet Mwita mmoja wa washiriki wa mafunzo yaliyofanyika hivi karibuni
katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Baadhi wa mafundi wa
Temesa kutoka mikoa mbalimbali nchini wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo
pichani) wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika
katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Mafundi wa TEMESA
wameshauriwa kutumia mafunzo waliyoyapata kuendana na mabadiliko ya teknolojia
katika utengenezaji magari na vifaa vya umeme.
Ushauri huo umetolewa
leo Jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Bodi ya Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA
Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri wakati wa hafla ya
kuhitimisha mafunzo kwa mafundi Wakala hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa
cha Usafirishaji (NIT).
Brigedia Jenerali
Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri amesema kuwa Serikali kupitia Wakala wa
Ufundi na Umeme TEMESA imedhamiria na kuhakikisha kuwa magari na mitambo yote
ya Serikali inatengenezwa kitaalam ili kuleta tija na thamani halisi ya fedha
iliyokusudiwa pamoja na kukidhi kiu na matarajio ya wateja.
”Napenda kuwakumbusha
kwamba mnayo dhamana kubwa ya kutengeneza magari ya Serikali hivyo kwa mafunzo
mliyoyapata ninaamini mmejenga uwezo wa kutosha wa kuhudumia magari na vifaa
vya umeme kwa kutumia mfumo wa kisasa” alisema Mhandisi Mashauri.
Ameongeza kuwa ni
fursa pekee kwa mafundi waliopata mafunzo hayo kwenda kuwafundisha wenzao ambao
hawakuweza kupata mafunzo hayo ili kuongeza kasi ya kutengenza magari na vifaa
vya umeme na kupunguza changamoto zilizopo katika utengenezaji magari kwa
kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Aidha Kaimu Mtendaji
wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan amewashukuru
washirika wa TEMESA wakiwemo Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kampuni
ya Superdoll kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo ambayo yataleta chachu ya
utendaji kazi wa mafundi na karakana za TEMESA zilizopo nchini nzima.
Wakala wa Ufundi na
Umeme TEMESA kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na
kampuni ya Superdoll waliandaa mafunzo ya siku 14 yaliyoanza Agosti
9 na kumalizika Agosti 26, 2016 yaliyoshirikisha jumla ya mafundi 25 kutoka
mikoa mbalimbali ili kuwapa uwezo wa kutengeneza magari kwa kutumia mifumo ya
kisasa.
No comments:
Post a Comment