Katibu
Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Benga’i Issa wa
kwanza kulia akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu maonesho ya
wajasiriamali yataofanyika Septemba 26 mwaka huu jijini Dar es salaam , kushoto
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini
(TPSF) Bw. Godfrey Simbeye.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye kushoto akiongea
na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu maonesho ya wajasiriamali yataofanyika
Septemba 26 mwaka huu jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Benga’i Issa.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama anatarajiwa kufungua maonesho
ya wajasiliamali yatofanyika Septemba 26 katika viwanja vya Mlimani City ambayo
yameandaliwa na Taasisi ya Ujasiriamali na ushindani Tanzania(TEEC) kwa
kushirikiana na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) pamoja na
Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ili kukuza uchumi wa nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa NEEC Bi. Beng’i Issa amesema kuwa
maonesho hayo yatalenga kuwawezesha wananchi kuwa wabunifu katika sekta ya
biashara ili kupiga hatua kufikia uchumi wa kati.
“Maonesho ambayo yatafanyika kesho
ni kwa ajili ya wajasiriamali wote wakubwa, wa kati na wadogo ili kuwawezesha
kiujuzi na kiushindani katika soko la biashara” alisema Bi. Issa.
Aidha Bi. Issa amesema kuwa siku
hiyo kutakuwa na kliniki ya biashara kwa watu wote kutoka kwa wataalamu wa
biashara ili kuweza kuwapatia mafunzo wajasiriamali wakubwa na wadogo ili
waweze kupata mafanikio yao na jamii kwa ujumla kupitia biashara zao.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye
amesema kuwa maonesho hayo yatawajengea wajasiriamali fursa za
masoko kwa biashara nchini na Afrika kwa ujumla.
“Kupitia maonesho hayo wajasiriamali
watapata fursa ya kutengeneza masoko ya biashara zao kwa ubora zaidi nchini na
afrika kwa ujumla ili waweze kujitangaza kimataifa” alisema Bw. Simbeye.
Aidha Bw. Simbeye amesema kuwa wana
mpango wa kuwaelimisha wajasiriamali kwa wingi zaidi ili waweze kuwa wabunifu
na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya biashara ndani na nje ya Tanzania.
Mbali na hayo Mkurugenzi Simbeye
amesema kuwa anawakaribisha watu wote wajasiriamali wakubwa na wadogo kufika
katika maonesho hayo ambayo hayana kiingilio ili waweze kupata ujuzi wa kutosha
kwa maendeleo ya biashara zao na kuinua uchumi wa nchi.
No comments:
Post a Comment