TIMU ya Mouloudia
Olympique Bejaia ya Algeria imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko
Veterani, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya wenyeji, Yanga mwishoni
mwa wiki.
Yanga watawakaribisha Mouloudia Olympique Bejaia Jumamosi katika mchezo wa marudiano Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga watawakaribisha Mouloudia Olympique Bejaia Jumamosi katika mchezo wa marudiano Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na timu hiyo ya Algeria imefikia kwenye hoteli ya Ledger Plaza, Kunduchi, Dar es Salaam, ambayo mara kadhaa wenyeji wao, Yanga huweka kambi na kufanya pia mazoezi Uwanja wa Boko.
Wachezaji
wa Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria wafanya mazoezi kwenye Uwanja wa
Boko Veterani, Dar es Salaam leo
Yanga bado haijaingia kambini na inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana, katikati ya Jiji tangu wiki iliyopita kujiandaa na mchezo huo.
Yanga itaingia katika mchezo wa jumamosi ikitoka kucheza mechi tano bila kushinda ikilazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa kirafiki, ikifungwa 1-0 mara mbili, na Mouloudia Olympique Bejaia nchini Algeria na TP Mazembe Dar es Salaam kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Medeama SC mjini hapa na baadaye kwenda kufungwa 3-1 na timu hiyo nchini Ghana katika mchezo wa marudiano.
Mara ya mwisho Yanga kushinda ilikuwa ni kwenye Fainali ya Kombe la TFF, ilipoibugiza Azam FC 3-1 Uwanja wa Taifa.
Yanga itahitimisha mechi zake za Kundi A Kombe la Shirikisho kwa kumenyana na wenyeji TP Mazembe ya DRC mjini Lubumbashi Agosti 23, mwaka huu.
Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi zake 10 baada ya mechi nne, ikishinda tatu na kutoa sare moja, ikifuatiwa na Bejaia na Medeama, ambazo kila moja ina pointi tano za sare tatu na ushindi mmoja, wakati Yanga inashika mkia kwa pointi yake moja.
No comments:
Post a Comment