Leo
August 25 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
leo amemteua Andrew Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Kabla ya uteuzi huo Bw. Andrew
Wilson Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu
Tanzania (BOT).
Andrew Wilson Massawe anachukua
nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus Francis Kipilimba ambaye ameteuliwa
kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Uteuzi wa Bw. Andrew
Wilson Massawe unaanza mara moja.
No comments:
Post a Comment