Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) imevuka lengo la ukusanyaji wa kodi wa jumla ya kiasi cha
shilingi trilioni 1 sawa na asilimia 95.6 tofauti na lengo lililokuwa
limekusudiwa la kukusanya trilioni 1.1 kwa mwezi Julai 2016.
Kiasi hicho ni sawa na
ongezeko la asilimia 15.43 ukilinganisha na makusanyo ya awali ya mwaka 2015
ambapo mamlaka hiyo ilikusanya jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 914.
Takwimu hizo
zimetolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard
Kayombo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jjijini Dar es Salaam.
“Kwa mwezi Julai mwaka huu makusanyo
yameongezeka kwa asilimia 15.43 ukilinganisha na kipindi cha mwezi Julai 2015
ambapo tulikusanya shilingi Bilioni 914” alisema Kayombo.
Aidha aliongeza kuwa
mamlaka imeweka mikakati thabiti ya kuhakikisha kuwa inafikia au inavuka lengo
la Serikali la kukusanya shilingi trilioni 15.1 kwa mwaka wa fedha 2016/2017
huku mkakati mmoja wapo ukiwa ni kuhakikisha kuwa walipa kodi wapya wanasajiliwa
zaidi.
Bw. Kayombo aliongeza
kuwa mkakati mwingine ni kuhuisha taarifa za walipa kodi kwa kuhakikisha kwamba
namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN) zisizotumika zinafutwa katika mfumo wa
TRA.
Pia amefafanua kuwa
maandalizi ya kuhuisha taarifa za walipa kodi yapo katika hatua za mwisho
ikiwemo upigaji picha,uchukuaji wa alama za vidole pamoja na vielelezo muhimu.
TRA inawakumbusha
wananchi kuhakikisha wanakagua tiketi/risiti zao za manunuzi na kuangalia
usahihi wa pesa walizolipa na uhalali wa risiti yenyewe.
No comments:
Post a Comment