Paul Pogba akiwa na jezi ya Manchester United kwa mara ya kwanza baada ya kukamilisha usajili wake usiku wa kuamkia leo
KLABU ya Manchester United imekamilisha uhamisho wa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Labile Pogba kwa dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 100 kutoka Juventus ya Italia.
Kiungo huyo aliyekuwa anatakiwa na timu nyingi kubwa duniani, ikiwemo Real Madrid, aliwasili kutoka Juventus jana na kujiiunga na klabu yakzamani, ambayo aliiacha mwaka 2012.
Kiungo huyo aliyekuwa anatakiwa na timu nyingi kubwa duniani, ikiwemo Real Madrid, aliwasili kutoka Juventus jana na kujiiunga na klabu yakzamani, ambayo aliiacha mwaka 2012.
Pogba mwenye umri wa miaka 23 anatarajiwa kuvaa jezi namba 6 na amesaini Mkataba mnono wa miaka mitano kwa mshahara wa Pauni 290,000 kwa wiki kufanya kazi chini ya kocha Mreno, Jose Mourinho.
Kuna kipengele pia cha kuongezwa mwaka mmoja katika Mkataba huo.
Akizungumza na tovuti ya klabu hiyo baada ya kusaini, Pogba alisema: "NIna furaha kujiunga tena na United. Imekuwa klabu yenye nafasi maalum katika moyo wangu wakati wote na ninaangalia mbele kuelekea kufanya kazi na Jose Mourinho.
"NImefurahia maisha yangu nikiwa na Juventus na nina kumbukumbu fulani nzuri za klabu kubwa na wachezaji ambao ninaweza kuhesabu kama marafiki. Lakini nafikiri ni wakati mwafaka kurejea Old Trafford.
"Wakati wote nafurahi kucheza mbele ya mashabiki na siwezi kusubiri kutoa mchango wangu kwenye timu. Hii ni klabu sahihi kwangu kushinda kitu chochote nachotumai kwenye mchezo,".
Kocha Jose Mourinho alimsifu Pogba na akasema anaamini atadhuhirisha thamani yake katuika urejeo wake kwenye klabu, akisema: "Paul ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani na atakuwa mtu muhimu katika timu ya United nayotaka kujienga hapa.
"Ni mwepesi, ana nguvu, anafunga mabao na anausoma mchezo vizuri kuliko wachezaji wengi. Akiwa ana umri wa miaka 23, ana nafasi ya kuifanya hiyo nafasi (kiungo) iwe ya kwake kwa miaka mingi hapa,"alisema Mourinho.
No comments:
Post a Comment