Vyombo
vya habari vya Marekani viliripoti kuwepo kwa mvutano baada ya Trump kurejea
matamshi yake ya kushambulia wazazi wa Mwanajeshi aliyeuawa nchini Iraq.
"Ningetaka
kuwafahamisha tu kwamba kampeni inaendelea vyema sana," amewaambia watu
waliohudhuria mkutano wake eneo la Daytona Beach.
Awali,
msaidizi mkuu wake Donald Trump Paul Manaford alikuwa pia amekana taarifa kuwa
kuna mgawanyiko mkubwa kwenye kampeni baada ya kile kinachodaiwa mfululizo wa
kauli za mgombea huyo wa chama cha Republican, zenye kukwaza.
''Kampeni
ziko vizuri, tumejipanga, tunasonga mbele,'' aliiambia kituo cha runinga cha
Fox News.
Baadhi
ya Maafisa wa Kampeni za Trump wamesema ''wanahisi kuwa wanapoteza muda wao''.
Hata
hivyo, Manafort amemlaumu mpinzani wa Trump wa Chama cha Democratic, Hillary
Clinton kwa ripoti hizo
''Hii ni kauli nyingine ya Clinton ambayo
imebebwa na vyombo vya habari, amesema ''Bwana Trump amejitokeza wiki hii kwenye
mikusanyiko mikubwa sana ya watu walifurika mpaka mtaani''.
Siku
ya Jumatano Bw Trump mwenyewe pia aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa
''kuna umoja kwenye Kampeni yangu, pengine mkubwa zaidi kuliko siku zote''.
Vita
vyake vya maneno na Khizr na Ghazala Khan, wazazi wa Kapteni Humayun Khan
aliyeuawa nchini Iraq, vimesababisha watu kutofautiana ndani ya Chama cha
Republican.
No comments:
Post a Comment