Baadhi ya Vijana wa mtaa wa Bugayambelele Kata
ya Lutede mkoani Geita wameshauriwa kuachana na michezo ya Pool table na kamali na badala
yake wajichanganye katika shughuli ndogo ndogo zitakazo waingizia kipato cha
halali.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Chama
cha mapinduzi Ccm tawi la Bugayambelele Bw Aniset Ngaiza wakati akizungumza na Mwandishi
wtu mtaani humo ambapo amesema vijana wengi katika eneo hilo hawataki kufanya
kazi kwa bidii na badala yake kushinda kwenye vijiwe vya pool table pamoja na
kamali.
Bw Ngaiza amesema chama cha mapinduzi Ccm
katika tawi hilo kimejipanga kuhakikisha kina washawishi baadhi ya vijana hao
kuendelea kuepuka michezo hiyo kwa kuwa nguvu ya kijana ni muhimu katika ujenzi
wa taifa.
Kwa upande wake katibu mwenezi wa chama cha
mapinduzi Ccm katika tawi hilo Bw Ally Bigambo amewashauri wazazi na walezi
kupunguza majukumu na kuwa karibu na watoto wao muda mwingi ili kuendelea
kuepuka kizazi kisicho penda kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment