Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa mradi wa
uunganishwaji umeme wa Gridi ya Taifa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye kituo
cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika Mkoani Lindi leo Mei 21, 2018.
Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Lindi, Godfrey Zambi. Mradi huo sasa umeondoa kero ya muda mrefu ya upatikanaji
wa umeme ulio bora na wa uhakika kwenye mikoa hiyo ya Kusini.
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa,(katikati) na viongozi wengine wa serikali wakiwemo mawaziri akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kuunganishwa umeme wa Gridi ya Taifa kwa
mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha
Mahumbika Mkoani Lindi leo Mei 21, 2018.
Waziri
Mkuu Majaliwa akimpongeza Waziri Dkt. Kalemani.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim
Majaliwa, (wapili kulia), akiwa na Viongozi wengine, wakiimba wimbo wa taifa
baada ya kufanya uzinduzi.
Waziri Mkuu Majaliwa, na viongozi wengine,
akipatiwa maelezo ya ,mradi huo na mmoja wa wataalamu wa TANESCO, kwenye kituo
cha Mahumbika.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akitoa hotuba yake
|
Waziri Mkuu Majaliwa, akitoa hotuba yake
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,
akitoa hotuba yake
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito
Mwinuka akitoa maelezo ya mradi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, akitoa
hotuba yake
Waziri Dkt. Kalemani (katikati), akisindikizwa
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,
Dkt. Tito Mwinuka
Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa amewahakikishia watanzania wote kuwa Serikali itafikisha umeme kila
kona na kila kijiji.
Waziri Mkuu aliyasema
hayo mara baada ya kuzindua mradi wa uunganishwaji wa umeme wa Gridi ya Taika
kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye hafla iliyofanyika Kituo cha kupoza na
kusambaza umeme cha Mahumbika mkoani Lindi leo Mei 21, 2018.
Hata hivyo aliwataka
kuwa wavumilivu kwani mipango ya serikali ambahyo ni kuhakikisha umeme unafika
sio tu maeneo ya mijini bali pia kwenye vijiji vyote vya Tanzania.
“Kitendo kinachofanyika
hapoa leo ni ushahjidi wa ahadi hiyo ya serikali na ninachowaomba Watanzania ni
kuwa na subira kwani serikali inatekeleza ahadi ilizotoa kuhakikisha watanzania
wanapata umem wa uhakika na wa bei nafuu.”
Akizungumzia uzinduzi
huo ambao sasa umetoa sukuhisho la uhaba wa umeme kwenye mkoa huo wa Lindi
Waziri Mkuu alitoa maagizo kwenye halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha
maeneo yote nyeti ya huduma za kijamii yanafikishiwa umeme ikiwemo shule na
hospitali
“Hatutarajii kuwa na
eneo lenye shida ya umeme, hapa ni umeme masaa 24, na tafsiri ya serikali kuwa
hapa ni umeme wa uhakika na wa kutosha ndio hii ambayo leo hii tumezindua.”
Alisema.
Alisema sera ya serikali
ni ya uchumi wa viwanda,na kwamba, wale watu wanaotaka kuwekeza viwanda vya
Korosho, Salfa na vifaa mbalimbaki kwenye mkoa wa Lindi sasa ni wakati wao
kwenda mkoani humo na kuwekeza kwani hivi sasa kuna umeme wa uhakika.
Aidha Waziri Mkuu
aliwaasa wananchi kuwa walizni wa miundombinu ya umeme, na kuwataka wanapoona
vitendo vya watu wakihujumu mkiundombinu basi taarifa za kuwashughulikia watu
hao ni vema zikatolewa kwa vyombo husika ili kuchukua hatua.
“Naomba vifaa vyote
vinavyoletwa kwenye maeneo yenu, kwenye vijiji vyenu basi tuvilinde ili
hatimaye tuweze kunufaika na uimarishwaji wa miundombinu ya umeme.” Aliasa
Wazir Mkuu.
Kupitia mpango w REA,
yaani umeme vijijini Serikali imepunguza kutoka Shilingi 380,000/= hadi
shilingi 27,000/= tu.
No comments:
Post a Comment