Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa amesema maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli ya kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji
ni sahihi na ameyafanya kwa wakati muafaka.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Bibi
Felista Bura (Viti Maalumu) aliyetaka kupata kauli ya Serikali juu ya baadhi ya
watu wanaobeza maamuzi ya Rais Magufuli ya kuupandisha hadhi mji huo.
“Pia Dodoma inajitosheleza kwa mahitaji mengi
ikiwemo uwepo wa taasisi mbalimbali muhimu kama Bunge la Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania, vyuo vikuu zaidi ya vitano, Ofisi ya UN, hivyo nampongeza
Mheshimiwa Rais Dkt Magufuli kwa uamuzi wake kwani unaleta tija kwa wananchi.
Nashauri jambo hili lipongezwe badala ya kubezwa,” Alisema Waziri Mkuu.
Aprili 26, 2018 Rais Magufuli aliupandisha
hadhi mji wa Dodoma kutoka Halmashauri ya Manispaa na kuwa Halmashauri ya Jiji
la Dodoma pamoja na kumteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw.
Godwin Kunambi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
No comments:
Post a Comment